Lugha Nyingine
Mapambano thabiti dhidi ya umaskini
Katika zaidi ya miaka 40 iliyopita tangu utekelezaji wa mageuzi na kufungua mlango ulipoanza, mafanikio makubwa yamepatikana katika maendeleo ya uchumi na jamii, ambapo mamilioni ya watu wameondokana na umaskini. Tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulipofanyika, China ilikuwa imelenga kwa usahihi watu wenye matatizo ya kiuchumi ili kuwasaidia wajiendeleze na kuondokana na umaskini. Serikali imeongeza uwekezaji, na kuwasaidia watu hao kwa njia mpya mbalimbali, ili hali mpya ionekane katika kazi ya kuondoa umaskini. Kuanzia mwaka 2013 hadi 2019, China ilikamilisha jukumu lake la kuwafanya watu waondokane na umaskini kuliko idadi iliyokuwa imepangwa. Ndani ya miaka hiyo saba, watu wenye matatizo ya kiuchumi wapatao milioni 93.48 waliondokana na umaskini, na idadi ya watu wenye matatizo ya kiuchumi ilipungua kutoka 10.2% hadi 0.6%, hayo ni mafanikio makubwa zaidi katika historia ya kuondoa umaskini nchini China. China imekuwa nchi iliyoondoa idadi kubwa zaidi ya watu wenye matatizo ya kiuchumi, pia ni nchi iliyotimiza kwanza malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa.
Kuwawezesha watu wenye matatizo ya kiuchumi na sehemu maskini kuingia pamoja na watu na sehemu zote nchini China kwenye jamii yenye maisha bora kwa pande zote, hii ni ahadi iliyotolewa kwa umakini na Chama cha Kikomunisti cha China. Ripoti ya Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China ilisema ni lazima kujipatia ushindi katika mapambano dhidi ya umaskini, na kuhamasisha nguvu ya Chama kizima, nchi nzima na jamii nzima kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiuchumi wajiendeleze ili kuondokana na umaskini, kufuata mpango wa jumla wa serikali kuu, ambapo kila mkoa, mji na wilaya itekeleze kihalisi utaratibu wa kazi, kuongeza nguvu ya kuwasaidia watu maskini, kuimarisha ushirikiano kati ya ukanda wa mashariki na ukanda wa magharibi katika kazi hiyo ya kupambana na umaskini, kuweka mkazo katika kusaidia sehemu zenye hali duni zaidi kuondoa umaskini, ili kuhakikisha watu wote maskini vijijini waondokane na umaskini, wilaya zote maskini ziondokane na umaskini, na kuondoa tatizo la umaskini wa kieneo kwa kigezo cha hivi sasa cha China ifikapo mwaka 2020.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma