Lugha Nyingine
Kuwasaidia watu maskini wajiendeleze na kulinda mazingira ya asili
Milima yenye ustawi wa miti na mito yenye maji safi ndiyo milima na mito ya dhahabu na fedha, hili ni wazo la Xi Jinping alilosisitiza mara kwa mara kuhusu kujenga ustaarabu wa mazingira ya asili. Wazo hilo linahusu majumuisho ya maarifa na mafunzo ya kihistoria katika maendeleo ya ustaarabu wa binadamu, limefikiria kwa kina umuhimu wa maendeleo ya binadamu, kufafanua vizuri suala gumu kuhusu uhusiano kati ya utafutaji wa watu juu ya maslahi ya kimali na mazingira ya asili wanayotegemea kuishi, na kuonesha hiari ya kiwango cha juu waliyonayo wakomunisti wa China juu ya ustaarabu na mazingira ya asili. Kushikilia kithabiti wazo kuhusu Milima yenye ustawi wa miti na mito yenye maji safi ndiyo milima na mito ya dhahabu na fedha, ndiyo kutoa kipaumbele kwa kulinda mazingira ya asili, na kujiendeleza bila kuchafua mazingira. Kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiuchumi wajiendeleze hakufai kusababisha uharibifu wa mazingira ya asili, ni lazima kutafuta njia mpya ya kujiendeleza ili kuondoa umaskini huku mazingira ya asili yakilindwa, na kuleta manufaa mengi zaidi kwa watu maskini katika kufufua na kulinda mazingira ya asili.
Kuwasaidia watu maskini wajiendeleze na kulinda mazingira ya asili, kunahusiana na mawazo mawili makubwa ya msingi: kwanza ni kutekeleza miradi ya kuleta maendeleo endelevu na kupatana na mazingira ya asili, kuzisaidia sehemu husika zitimize maendeleo ya uchumi, na kutoharibu mazingira ya asili. Pili ni kuchukulia mazingira ya asili kuwa ni raslimali inayoweza kutumiwa kwa ufanisi katika kusaidia kazi ya kuondoa umaskini, ili kutimiza lengo la kupata maendeleo ya kiuchumi, kuboreshwa kwa maisha ya watu na kulinda mazingira ya asili ya sehemu zinazohusika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma