Lugha Nyingine
Jinsi hekaya za kale zinavyomithilisha vizuri usafiri wa China kwenye anga ya juu kwa hivi sasa
By Sheng Shuang, Liu Dong, Zhou Linjia, Song Ge, Cao Yuhan (mwanafunzi anayefanya mazoezi)
Maana ya majina ya vyombo vya China vya safari kwenye anga ya juu
Katika wakati wa kutoa majina kwa ya vyombo vya China vya safari kwenye anga ya juu, “Xihe”, ni jina la satelaiti ya kutafiti sayari ya Jua, jina hilo ni la mungu wa kike wa Jua kwenye hekaya ya zama za kale za China ; “Chang’e”, ni jina la mradi wa China wa kutafiti sayari ya Mwezi, hilo ni jina la malaika katika hekaya ambaye aliruka na kuelekea sayari ya Mwezi; na, kigari cha kutafiti sayari ya Mars limepewa jina la Zhurong, ambalo ni jina la mungu wa moto wa awali kabisa katika hekaya......teknolojia ya hali ya juu ya safari ya anga ya juu ya China ikihusiana na utamaduni wa China imenga’ra zaidi na kuzifanya hadithi simulizi za zama za kale ziingie katika hali halisi ya hivi sasa.
Chang’e——Mradi wa China wa Kutafiti Sayari ya Mwezi
Yutu——Kigari cha Mwezi
Queqiao——Satelaiti ya Kupokea na Kurushia Ujumbe
Tianwen—Mradi wa China wa kufanya utafiti juu ya sayari
Zhurong—kigari cha utafiti wa sayari ya Mars
Xihe—satelaiti ya majaribio ya kisayansi na kiteknolojia ya kutafiti sayari ya Jua
Shenzhou——Chombo cha kubeba binadamu kwenye safari ya anga ya juu kilichosanifiwa na kutengenezwa na China yenyewe
Tiangong——kituo cha China cha kubeba binadamu kwenye anga ya juu
Wukong——satelaiti ya kutafiti chembechembe za vitu visivyoonekana
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma