Lugha Nyingine
Rais wa China ajibu barua ya rais wa IOC Thomas Bach
Rais Xi Jinping wa China amejibu barua iliyoandikwa na rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach.
Katika barua yake, Rais Xi ameeleza kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022 imemalizika kwa mafanikio, na China imetekeleza kikamilifu ahadi yake kwa kuandaa Michezo ya Olimpiki iliyozingatia kubana matumizi ya fedha, usalama na mizuri, na kusifiwa sana na jumuiya ya kimataifa.
Rais Xi amemshukuru Bw. Bach na IOC kwa kuunga mkono kithabiti Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, akieleza kuwa serikali ya China inapenda kudumisha ushirikiano wa karibu na IOC, kuendelea kuunga mkono kazi ya IOC, kufuata moyo wa Olimpiki, kuhimiza kwa pamoja maendeleo ya michezo ya Olimpiki, na kuandika kwa pamoja ukurasa mpya wa ujenzi wa Jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma