Lugha Nyingine
Xi Jinping awahamasisha vijana kuchangia zaidi kwenye sekta ya anga ya juu ya China
(CRI Online) Mei 05, 2022
Rais Xi Jinping wa China amewahamasisha vijana waliopo kwenye sekta ya anga ya juu kutoa mchango zaidi kwenye sekta ya utafiti wa anga ya juu na kutimiza uwezo wa kujitegemea zaidi kupitia uvumbuzi kwenye sekta ya sayansi na teknolojia ya anga ya juu ya China.
Rais Xi ameyasema hayo Jumatatu kwenye barua aliyoituma kwa timu ya vijana ya ujenzi wa kituo cha anga ya juu kwenye Shirika la Sayansi na Teknolojia ya Anga ya Juu la China (CASC) kabla ya Mei 4 ambayo ni Siku ya Vijana ya China. Rais Xi amesema mambo ya anga ya juu ya China yanazidi kupata maendeleo mapya, na vijana wengi kwenye sekta hiyo wamefanya kazi ya uongozi wakibeba majukumu muhimu, ambao wameonyesha ujasiri wa vijana wa China wa kusonga mbele katika zama mpya.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma