Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China atoa amri ya kumpandisha cheo ofisa wa kijeshi hadi cheo cha jenerali
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikabidhi cheti cha amri kwenye hafla ya kumpandisha cheo kamanda wa Kamandi ya Theatre ya Kaskazini ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), Wang Qiang, kuwa jenerali, hapa Beijing, China, Septemba 8, 2022. Hafla hiyo imeandaliwa na CMC mjini Beijing. (Xinhua/Li Genge)
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), Alhamisi wiki hii alikabidhi cheti cha amri kwenye hafla ya kumpandisha cheo kamanda wa Kamandi ya Theatre ya Kaskazini ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), Wang Qiang, kuwa jenerali.
Hafla hiyo imeandaliwa na CMC mjini Beijing. Cheo cha Jenerali ndiyo daraja la juu zaidi kwa maofisa wa jeshi wanaofanya kazi kwa bidii nchini China.
Katika hafla hiyo, Xi alitoa pongezi zake kwa Wang, ambaye alimsalimia Xi na washiriki wote kwenye hafla hiyo.
Xu Qiliang, Naibu Mwenyekiti wa CMC, alitangaza amri ya kupandishwa cheo kwa Wang katika hafla hiyo iliyoongozwa na Naibu Mwenyekiti wa CMC Zhang Youxia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma