超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Habari Picha: Viwanja vya Michezo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Joto ya Chengdu vinavyobeba “Mtindo wa Sichuan”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 19, 2023

Mashindano ya 31 ya Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya FISU yatafunguliwa Chengdu, China Julai 28. Jumla ya miundombinu 45 ya mashindano itatumika kwa ajili ya mazoezi ya utayari na mashindano hayo. Huku muda wa mashindano hayo ukiwa umebaki siku 100 pekee, pata kutazama baadhi ya miundombinu ya kuvutia iliyosanifiwa na kujengwa kwa "mtindo wa Sichuan" Mkoa wa China ambao mji wa mashindano hayo wa Chengdu unapatikana.

Uwanja wa Bustani ya Michezo ya Ziwa Dong'an

(Picha kwa hisani ya Chengdu 2021)

(Picha kwa hisani ya Chengdu 2021)

Sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Vyuo Vikuu Duniani ya Chengdu 2021 FISU zitafanyika katika uwanja huu. Uwanja huo ukiwa uwanja mkuu wa michezo katika Bustani ya Michezo ya Ziwa Dong'an, ni uwanja wenye umbo la "fedha frisbee" ulioko katika Eneo la Longquanyi la Chengdu, una uwezo wa kuchukuka watu 40,000 na eneo lake ni la mita za mraba 120,000.?

(Picha na Xinhua/Shen Bohan)

(Picha na Xinhua/Shen Bohan)

Uwanja huo wenye kimo cha mita 50 unatimiza masharti ya uendeshaji yanayohitajika kwa ajili ya kuandaa hafla za kufunguliwa na kufungwa kwa michezo au mkutano mkubwa, kwa kuwa na eneo lake la mapokezi la kiwango cha juu la VIP na jukwaa la kutazama lenye umbo la upinde wa kimo cha Mita 29 , na urefu wa Mita 300.?

 (Xinhua/Shen Bohan)

(Xinhua/Shen Bohan)

Uwanja huu ndiyo mkubwa zaidi kati ya viwanja vitatu vilivyo karibu na uwanja huo mkuu. Uwanja huu wa michezo wenye eneo la mita za mraba 90,169.37 hutumika kama uwanja wa mashindano na mazoezi ya michezo ya Sanaa ya jeminestik.

Uwanja wa Matumizi mengi wa Bustani ya Michezo ya Ziwa Dong'an Lakehttps://english.news.cn/20230418/ad9ca160dd794839b7b69817bb72aff2/20230418ad9ca160dd794839b7b69817bb72aff2_bab2b697-59a7-4d24-8b8a-bca5c9bbca01.png

Huu ni mwonekano wa ndani ya Kituo cha Michezo ya Kuogelea katika Bustani ya Michezo ya Ziwa Dong'an.

Kituo hicho kina eneo la mita za mraba 73,549.33. Wakati wa Michezo ya Chengdu 2023 , kituo hicho kitatumika kwa mashindano, kupasha misuli joto na kufanya mazoezi kwa michezo ya kuogelea. Jumla ya medali 42 za dhahabu katika michezo ya kuogelea zitatolewa hapa kuanzia Agosti 1 hadi 7.

Uwanja wa Michezo wa Bustani ya Fenghuangshan

https://english.news.cn/20230418/ad9ca160dd794839b7b69817bb72aff2/20230418ad9ca160dd794839b7b69817bb72aff2_1f7b2465-cc9d-4a5c-92b2-fca0fe149796.png

Huu utakuwa kivutio cha mashabiki wa mpira wa wavu wakati wa Michezo, kwani medali mbili za dhahabu katika michezo ya mpira wa kikapu zitatolewa hapa. Uwanja huo ulioko katika Eneo la Jinniu la Chengdu ni uwanja mkubwa zaidi wenye eneo la mita za mraba 119,704.76, lenye ghorofa saba juu ya ardhi na ghorofa moja chini ya ardhi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha