Lugha Nyingine
Rais wa China ahutubia Mkutano wa Kilele wa Ukanda Mmoja, Njia Moja
(Picha inatoka Xinhua.)
Mkutano wa Kilele wa Tatu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja umefunguliwa leo tarehe 18 Oktoba mjini Beijing.
Akihutubia mkutano huo, rais Xi Jinping wa China amesema binadamu ni jamii yenye mustakabali wa pamoja, na ushirikiano wa kunufaishana ni njia ya uhakika ya kufanikiwa katika kuanzisha mipango mikuu inayowanufaisha wote.
Ameeleza kuwa nchi zinapokumbatia ushirikiano na kuchukua hatua kwa pamoja, pengo kubwa linaweza kugeuzwa kuwa njia ya kupita, nchi zisizo na bahari zinaweza kuunganishwa na bahari, na mahali penye maendeleo duni panaweza kugeuzwa kuwa nchi ya ustawi.
Rais Xi amesema, kusaidia wengine ni sawa na kujisaidia mwenyewe, na kwamba kuona maendeleo ya wengine kama tishio au kuchukulia kutegemeana kiuchumi kama hatari hakutafanya maisha ya mtu kuwa bora zaidi au kuharakisha maendeleo yake.
Rais Xi ametangaza kuwa, pamoja na washirika wake wa ushirikiano, China itatoa Mafanikio na Matarajio ya Ujenzi wa Dhati wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Kanuni za Ngazi ya Juu za Ujenzi wa Dhati wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kuanzisha Mfumo wa Tathmini na Uzingatiaji wa Makampuni Yanayohusika katika Ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja. Pia amesema China itashirikiana na mashirika ya kimataifa kufanya utafiti na mafunzo ya kukuza udhati katika ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.
Aidha amesema China itaendelea kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kushirikiana na washirika wa BRI kuimarisha ujenzi wa majukwaa ya ushirikiano wa pande nyingi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma