Lugha Nyingine
Maoni: Kuweka dira mpya ya uhusiano wa China na Vietnam katika zama mpya
Kutokana na mwaliko wa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam Nguyen Phu Trong na Rais wa Jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam Vo Van Thuong, Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), atafanya ziara ya kiserikali nchini Vietnam kuanzia Desemba 12 hadi 13.
Hii ni mara nyingine tena kwa Rais Xi kutembelea Vietnam baada ya miaka sita iliyopita, na ziara hii imeendelea kufuata desturi nzuri ya viongozi wa vyama na nchi hizo mbili kutembeleana mara kwa mara kama ndugu. Hasa ziara hii ni muhimu katika wakati wa maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Vietnam. Pande hizi mbili China na Vietnam zimefikia makubaliano ya kupandisha tena hadhi ya uhusiano wao na kuongeza ushirikiano wa kufuata hali halisi kati ya pande mbili, na kuweka dira ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Vietnam. Kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye umuhimu wa kimkakati ya China na Vietnam ya mustakabali wa pamoja na kuweka dira ya maendeleo ya uhusiano wao katika zama mpya, hakika ziara hiyo itakuwa mnara kwenye historia ya uhusiano wa China na Vietnam.
Hivi sasa uhusiano wa nchi hizo mbili umepata maendeleo makubwa chini ya uelekezaji wa misingi ya “majirani wema, marafiki wazuri, makomredi wazuri na washirika wazuri" . Katika miaka mingi iliyopita, viongozi wa ngazi ya juu wa vyama na nchi za China na Vietnam wamedumisha mawasiliano ya karibu na kutembeleana mara kwa mara kupitia njia mbalimbali, wakiendeleza urafiki wa dhati wa “makomredi na ndugu” kati ya nchi hizo mbili, hali ambayo imekuwa simulizi nzuri ya uhusiano wa kimataifa kwa hivi sasa.
China na Vietnam ni washirika muhimu wa kibiashara. China imekuwa mshirika mkubwa wa kwanza wa kibiashara wa Vietnam kwa miaka mingi mfululizo, na Vietnam imekuwa mshirika mkubwa wa nne wa kibiashara wa China. Thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili imezidi Dola za Marekani bilioni 200.
Njia ya mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Vietnam inapanuliwa siku hadi siku. Katika mipaka kati yao, wakazi, wafanyabishara na watalii wengi wanawasiliana kila wakati; Katika vyuo vikuu vya pande zote mbili, vijana wengi zaidi wa kila upande wanakwenda upande mwingine kusoma na kujifunza lugha husika; katika mtandao wa intaneti, vijana wengi zaidi wa kila upande wanatazama na kupenda programu za televisheni na filamu kutoka pande zote mbili.
Katika ziara hii, China na Vietnam zitaweka mkazo kwenye maeneo sita muhimu ya siasa, usalama, ushirikiano wa kivitendo, msingi wa maoni ya umma, ushirikiano wa pande nyingi na mambo ya baharini, kuhimiza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote wa nchi hizo mbili kuwa wa kina na imara zaidi, na kujenga siku nzuri za baadaye zenye mustakabali wa pamoja.
(Makala hii imeandikwa na mtafiti wa Kituo cha Utafiti wa Wazo la Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye Umaalumu wa China katika Zama Mpya, kituo ambacho ni chini ya Taasisi Kuu ya Sayansi ya Jamii ya China.)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma