Lugha Nyingine
Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa maadhimisho ya miaka 50 ya kamati ya taifa ya biashara ya Marekani na China
Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa kamati ya taifa ya biashara ya Marekani na China, akitoa pongezi kwa kamati na wajumbe wake wote na salamu za dhati kwa watu wa jamii mbalimbali za Marekani wanaofuatilia na kuunga mkono ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani.
Amesema wakati Dunia ikikabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajapata kushuhudiwa katika miaka mia moja iliyopita, kuungana mikono na kushirikiana kwa China na Marekani katika kukabiliana na changamoto kwa pamoja au la kunahusiana na maslahi za nchi mbili na kuathiri mustakabali wa binadamu wote.
Amesema, kabla ya hapo, alikutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden huko San Francisco, na kubadilishana naye maoni kuhusu masuala makubwa ya uhusiano kati ya China na Marekani na kufikia makubaliano muhimu.
Amesema China iko tayari kushikilia kanuni za kuheshimiana, kuishi kwa amani, ushirikiano wa kunufaishana, na kufanya juhudi pamoja na Marekani kutekeleza makubaliano ya San Francisco, ili kuhimiza maendeleo chanya, endelevu na tulivu ya uhusiano kati ya China na Marekani.
Wakati huohuo, Rais Joe Biden wa Marekani pia ametuma barua ya pongezi kwa hafla ya maadhimisho hayo ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa kamati ya taifa ya biashara ya Marekani na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma