Lugha Nyingine
Mji wa Beijing, China washuhudia ustawishaji wa tasnia za kitamaduni, na kuvunja rekodi kadhaa
Picha hii iliyopigwa Desemba 25, 2023 ikionyesha ukumbi wa muziki wa Kituo cha Sanaa za Maonyesho cha Beijing, China. (Xinhua/Peng Ziyang)
BEIJING – Mji wa Beijing, China umeshuhudia kuimarika kwa kasi kubwa katika tasnia za utamaduni Mwaka 2023, ikisajili idadi inayovunja rekodi ya maonyesho ya bidhaa na maonyesho ya burudani za jukwaani ya kibiashara, amesema Huo Zhijing, Naibu Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Beijing siku ya Jumatatu.
Katika mwaka mzima wa 2023, maonyesho ya burudani za jukwaani ya kibiashara zaidi ya 49,000 yalifanyika Beijing, ambayo mauzo ya tiketi zenye thamani ya yuan zaidi ya bilioni 2.3 (kama dola za Kimarekani milioni 323.41), huku takwimu zote mbili zikiweka rekodi mpya. Idadi ya maonyesho imeongezeka maradufu ikilinganishwa na idadi hiyo kabla ya UVIKO-19 katika Mwaka 2019.
"Beijing imepiga hatua kubwa katika kujiendeleza na kuwa kitovu cha sanaa za maonyesho ya jukwaani," afisa huyo amesema.
Mwaka jana, Beijing pia ilijitahidi kujijenga kuwa "mji wa makumbusho" kwa kuongeza makumbusho 11 mapya yaliyosajiliwa na taasisi 27 zinazofanana na makumbusho. Maonyesho ya kazi za Sanaa zaidi ya 700 yalifanyika, yakiashiria rekodi ya juu, na kuvutia idadi inayovunja rekodi ya watembeleaji milioni 87.
Kuanzia Januari hadi Novemba 2023, tasnia za utamaduni za Beijing zilipata mapato ya jumla yanayozidi Yuan trilioni 1.8, ikiwa ni ongezeko kubwa la mwaka hadi mwaka la asilimia 14, Huo ameongeza.
Afisa huyo ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari wa mkutano wa mwaka unaoendelea wa Bunge la Umma la Beijing.
Katika Picha: Maonyesho ya taa za kijadi ya bustani ya Yuyuan mjini Shanghai, China
Watu washerehekea Sikukuu ya Timket huko Addis Ababa, Ethiopia
Sehemu ya pili ya mradi wa jengo la Kituo cha Mambo ya Fedha cha Nanjing wawekewa vifuniko
Umoja wa Mataifa kuchapisha stempu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2024
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma