Lugha Nyingine
Makumbusho ya Uingereza kurudisha hazina za kale za kifalme za Ghana
Jumba la Makumbusho la Uingereza na Jumba la Makumbusho la Victoria na Albert yatarudisha vitu vya kale vya dhahabu na fedha vilivyoporwa wakati wa ukoloni kutoka kwenye mahakama ya kifalme ya Himaya ya Kale ya Asante ya Ghana.
Makubaliano hayo ya Ghana ya kuchukua vitu hivyo vya kale kwa mkopo wa muda mrefu yanakuja huku shinikizo ya kimataifa ikiongezeka kwa majumba ya makumbusho na taasisi kurejesha vitu vya kale vya Afrika kutoka kwa mataifa yenye nguvu ya kikoloni yakiwemo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Ubelgiji.
Bidhaa zilizorejeshwa kwa Ghana chini ya makubalino ya mkopo huo ni pamoja na upanga wa Mponponso wenye umri wa miaka 300 uliotumika katika sherehe za kuapishwa Mfalme wa Himaya ya Asante, Asantehene, paipu ya amani ya dhahabu na beji za dhahabu za kutakasa roho, miongoni mwa hazina nyinginezo.
Mabaki hayo yalichukuliwa baada ya Vita vya tatu vya Anglo-Asante mwaka 1874 na yanajumuisha vitu 32, 15 kutoka Makumbusho ya Uingereza na 17 kutoka Makumbusho ya Victoria na Albert, ambayo yote yako London.
Ikulu ya kifalme imesema vitu hivyo vitaoneshwa huko Kumasi, makao ya Ufalme wa Asantehene, kwenye Jumba la Makumbusho la Ikulu ya Manhyia kwa hadi miaka sita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma