Lugha Nyingine
Wilaya ya Caoxian: Kueneza uzuri wa China na kuhimiza wimbi la mavazi ya kijadi ya Hanfu ya Kabila la Wahan
Katika miaka ya hivi karibuni, viwanda vya mavazi ya kijadi ya Hanfu ya Kabila la Wahan katika Wilaya ya Caoxian ya Mji wa Heze, Mkoa wa Shandong, China vimeendelea kwa kasi. Ingawa vilianza kwa kuchelewa, lakini kwenye msingi wa viwanda vyake vya kutengeneza mavazi na mapambo ya maonesho ya michezo ya Sanaa na nguvu yake ya biashara ya mtandaoni, uzalishaji wa mavazi ya Hanfu ya Caoxian umeendelea kwa kasi na sasa umechukua 40% ya soko lote la China, na wilaya ya Caoxian imekuwa kituo kikubwa zaidi cha uzalishaji wa mavazi ya Hanfu nchini China.
Mwaka Mpya wa Jadi wa China unapokaribia, seti ya mavazi ya "blauzi ya salamu za Mwaka Mpya + sketi ya uso wa farasi" yanayozalishwa hapa ni adimu sokoni na inapendwa sana na wateja.
Mteja akichagua mavazi ya kabila la Wahan kwenye kituo cha kutangaza na kuuza bidhaa moja kwa moja mtandaoni cha bohari ya Youai katika Wilaya ya Caoxian iliyoko Mji wa Heze, Mkoa wa Shandong, China, tarehe 23, Januari. (Picha na Zhou Linjia/People's Daily Online)
Uchumi huo wa mavazi ya Hanfu unaoshamiri sana siyo tu umehamasisha idadi kubwa ya vijana kurejea katika miji yao walikozaliwa kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji wa mavazi, bali pia kutumia vilivyo nguvukazi ya ziada ya eneo hilo. Wanawake na wazee ambao walikuwa wakiangalia na kuhudumia watoto wao nyumbani sasa wanaweza kusaidia kutengeneza nguo, kushona vifungo, na kupata mapato yao wenyewe.
Muundo unaoendelea kuboreshwa wa biashara ya mtandaoni umesaidia wilaya hiyo ya kilimo cha jadi kujiondoa haraka kutoka kwenye umaskini. "Kila familia inafungua duka la mtandaoni na kila mtu anaelewa biashara ya mtandaoni." Hali ya kushamiri kwa biashara ya mtandaoni hapa pia imekuwa nguvu kuu ya uendeshaji na msingi wa ushindani wa maendeleo ya haraka ya viwanda vya mavazi vya Hanfu katika wilaya hiyo.
Hebu tufuatilie na kujua simulizi ya uchumi unaostawi wa mavazi ya Hanfu hapa pamoja na wanahabari wa People's Daily Online!
Balozi: China imejikita katika kuendeleza uhusiano wa pande mbili na Ethiopia
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma