Lugha Nyingine
Marais wa China na Angola wafanya mazungumzo na kuinua uhusiano wa pande mbili kuwa wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote
Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Angola Joao Lourenco katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Machi 15, 2024. (Xinhua/Li Xueren)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping alifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Angola Joao Lourenco, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, mjini Beijing siku ya Ijumaa ambapo viongozi wakuu hao wawili wa nchi wametangaza kuinua uhusiano wa pande mbili kuwa wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote.
Rais Xi amesema kuwa China na Angola mwaka jana ziliadhimisha pamoja miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umestahimili majaribu ya mabadiliko ya kimataifa na kunufaisha watu wa nchi hizo mbili.
Rais Xi amesema, Ushirikiano kati ya China na Angola ni ushirikiano wa Kusini-Kusini na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea, ambao ni kuhusu kusaidiana, kunufaishana na kufanya ushirikiano, na kutafuta maendeleo kwa pamoja kati ya marafiki wazuri. Katika hali ambayo dunia inakabiliwa na mabadiliko na misukosuko, pande hizo mbili zinapaswa kuendeleza urafiki wao wa jadi, kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kuungana mkono kwa uthabiti, ili kufikia maendeleo kwa pamoja.
Amesema China inaunga mkono Angola katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo yake ya kitaifa, kutafuta njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa inayoendana na hali halisi ya nchi yake, na kufikia maendeleo na ustawishaji wa taifa.
China pia ingependa kuimarisha mabadilishano ya uzoefu wa utawala wa nchi na Angola, kupandisha hadhi ya uhusiano wa kimkakati wa pande mbili, na kuhimiza kwa pamoja mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa wa kila nchi, Rais Xi ameeleza.
Amesema China ingependa kufanya juhudi pamoja na upande wa Angola katika kutekeleza vizuri miradi muhimu ya miundombinu, kuunga mkono kampuni za China zenye uwezo kufanya ushirikiano wa aina mbalimbali nchini Angola, na kuisaidia nchi hiyo kuendeleza kilimo cha kisasa, kuendeleza viwanda na kukuza uchumi wa aina mbalimbali.
Rais Xi ametumai kuwa Angola itachukua hatua madhubuti zaidi ili kuhakikisha haki na maslahi halali na usalama wa raia na kampuni za China. Angola inakaribishwa kutambulisha bidhaa bora nyingi zaidi nchini China kwa kupitia Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji na Uuzaji nje Bidhaa ya China na Maonyesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika.
Rais Lourenco amesema kuwa China ilikuwa nchi ya kwanza kutoa usaidizi muhimu wakati Angola ilipokuwa inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na ikipambana na janga la UVIKO-19, na ametoa shukrani zake za dhati.
"Uungaji mkono na ushirikiano wa China umewezesha sana ujenzi wa miundombinu na maendeleo ya uchumi na jamii ya Angola, na kuwa mfano mzuri wa ushirikiano wa kunufaishana," ameongeza Lourenco.
Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Angola Joao Lourenco katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Machi 15, 2024. (Xinhua/Li Xueren)
Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Angola Joao Lourenco katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Machi 15, 2024. (Xinhua/Ding Lin)
Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Angola Joao Lourenco katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Machi 15, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Angola Joao Lourenco ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing mjini Beijing, China, Machi 15, 2024. (Xinhua/Ding Lin)
Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Jamhuri ya Angola Joao Lourenco kwa pamoja wakishuhudia hafla ya utiaji saini wa nyaraka kadhaa za ushirikiano wa pande mbili kuhusu ushirikiano wa ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ushirikiano katika sekta za uchumi na biashara, kilimo, na maendeleo ya kijani baada ya mazungumzo yao kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 15, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma