Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asisitiza kujenga vyuo vikuu vya matibabu vya jeshi vya kiwango cha juu duniani
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akifahamishwa kuhusu vifaa vinavyotumika kwa matibabu kwenye uwanja wa vita na kielelezo cha kufanyika kwa matibabu katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Jeshi, Aprili 23, 2024. (Xinhua/ Li Gang)
CHONGQING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika Chuo Kikuu cha Matibabu cha Jeshi siku ya Jumanne ametoa wito wa kujenga vyuo vikuu vya matibabu vya jeshi vya kiwango cha juu duniani, akisisitiza kwamba vinapaswa kuhudumia uwanja wa vita na askari, na kukumbatia siku za baadaye.
Akisisitiza haja ya kutekeleza mawazo ya kuimarisha jeshi katika zama mpya, Rais Xi amehimiza chuo kikuu hicho kuboresha uendeshaji wake na uendelezaji wa vipaji, na kuongeza uwezo wa kuhakikisha matibabu na huduma wakati wa vita. Kwenye ziara hiyo ya ukaguzi, Rais Xi amefahamishwa kuhusu hali ya kimsingi ya chuo kikuu hicho na taaluma muhimu kuhusu huduma ya matibabu kwenye uwanja wa vita.
Tokea kupangwa upya na kuanzishwa Mwaka 2017, chuo kikuu hicho kimekamilisha msururu wa kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha matibabu na huduma wakati wa mapambano ya kijeshi na kuzuia na kudhibiti UVIKO-19. Rais Xi ametambua juhudi za chuo kikuu hicho katika kuhimiza maendeleo na kukamilisha kazi.
Rais Xi alikutana na wajumbe wa maofisa na askari wa chuo kikuu hicho na kupiga nao picha ya pamoja.
Amesisitiza umuhimu wa kujenga uadilifu na kuendeleza uwezo wa kupambana, na pia kuhimiza uvumbuzi kwa hamasa kubwa katika utafiti wa kisayansi wa tiba wa kijeshi ili kupata nafasi ya juu zaidi katika maendeleo ya nyanja hiyo.
Rais Xi amesisitiza Chama kujiendesha kwa nidhamu kali na kutoa elimu ya nidhamu ya Chama.
Kazi inapaswa kufanywa ili kuendeleza utawala wa kufuata sheria na kuimarisha usimamizi wa elimu, na ameagiza kufanya juhudi kwa pamoja ili kufungua upeo mpya wa maendeleo ya chuo kikuu hicho.?
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikutana na wajumbe wa maofisa na askari wa Chuo Kikuu cha Matibabu cha Jeshi na kupiga picha nao, Aprili 23, 2024. (Xinhua/ Li Gang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma