Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China aeleza msimamo wa China juu ya mapambano kati ya Paletina na Israel na mgogoro wa Ukraine
Rais Xi Jinping wa China na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wakihudhuria kwa pamoja kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Paris, Ufaransa, Mei 6, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)
Rais Xi Jinping wa China ameeleza msimamo wa China kuhusu mapambano kati ya Palestina na Israel na mgogoro wa Ukarine wakati alipohudhuria kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Paris siku ya Jumatatu.
Mapambano uliodumu kwa muda mrefu kati ya Palestina na Israel ni jaribio kwa maadili ya binadamu, na jumuiya ya kimataifa lazima ichukue hatua, alisema Xi.
China inatoa wito kwa pande zote kufanya juhudi ili kusimamisha vita mara moja, kwa pande zote na kwa njia endelevu katika Gaza, alisema, akiongeza kuwa China inaunga mkono Palestina kuwa nchi mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa, na kuunga mkono kurejesha mamlaka halali ya Paletina na kuanzisha tena utatuzi wa nchi mbili, ili kutimia amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati.
Xi alisisitiza kuwa China imeeleza msimamo wake juu ya mgogoro wa Ukraine mara kwa mara.
China haikuchochea mgogoro wa Ukraine, wala si pande husika na inayoshiriki kwenye mgogoro huo, alisema Xi, akisema kuwa badala ya kuwa mtazamaji tu, China imefanya umuhimu wake katika kujenga amani.
Wajumbe maalumu wa serikali ya China wanaoshughulikia mambo ya Ulaya na Asia wanafanya jitihada za kidiplomasia za raundi ya tatu, aliongeza.
Wakati huo huo, China inapinga vitendo vya kutumia mgogoro wa Ukraine kusingizia upande wa tatu, kuupakia matope nchi nyingine, na kuchochea “Vita Mpya ya Baridi,” alisema.
Rais Xi Jinping wa China na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wakihudhuria kwa pamoja kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Paris, Ufaransa, Mei 6, 2024. (Xinhua/Li Xueren)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma