Lugha Nyingine
Marais wa China na Hungary wafanya mazungumzo
Rais Xi Jinping wa China na rais Tamas Sulyok wa Hungary wamefanya mazungumzo katika Ikulu ya rais huko Budapest asubuhi ya tarehe 9, Mei.(Picha na Zhai Jianlan/Xinhua)
Rais Xi Jinping wa China na rais Tamas Sulyok wa Hungary wamefanya mazungumzo katika Ikulu ya rais huko Budapest.
Katika mazungumzo hayo, Rais Xi ameeleza kuwa huu ni mwaka wa 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Hungary. China inapenda kushirikiana na Hungary, kuenzi urafiki wa kijadi, kukuza kuaminiana kisiasa, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, na kuongoza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupanda katika ngazi ya juu zaidi.
Kwa uapnde wake Rais Sulyok ameeleza kuwa, Hungary inatarajia kukuza mawasiliano na China, kuimarisha uunganishaji wa mikakati ya maendeleo, na kuhimiza miradi muhimu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili. Pia anaamini kuwa ziara hiyo ya kihistoria ya Rais Xi itahimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya Hungary na China kupanda katika kiwango cha juu zaidi.
Rais Xi Jinping wa China na rais Tamas Sulyok wa Hungary wamefanya mazungumzo katika Ikulu ya rais huko Budapest asubuhi ya tarehe 9, Mei.(Picha na Zhai Jianlan/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma