Lugha Nyingine
Msaada wa thamani wa Xi Jinping ulivyobadilisha hatima ya jengo lililojengwa miaka 110 iliyopita
Jengo la Bagualou lenye historia ya zaidi ya miaka 110, ni moja ya alama za majengo kwenye Kisiwa cha Gulangyu. Wakati Rais Xi Jinping wa China alipokuwa akifanya kazi katika Mji wa Xiamen, Mkoa wa Fujian wa China alisaidia kubadilisha hatima ya jengo hilo lililojengwa zamani sana.
Jengo la Bagualou liko katika sehemu ya kaskazini-mashariki ya Mlima Bijia, kaskazini-mashariki mwa Kisiwa cha Gulangyu, ambapo likitazamana na Bandari ya Xiamen, China. (Picha na Xu Qiuheng)
Kisiwa cha Gulangyu kinajulikana kuwa ni "Makumbusho ya Majengo ya Mataifa Yote". Likiwa ni eneo la kitaifa la ulinzi wa mabaki ya kitamaduni, Jengo la Bagualou ni moja ya mambo ya msingi ya mali ya urithi wa kitamaduni wa dunia wa Kisiwa cha Gulangyu. (Picha na Yang Jinjian)
Jengo la Bagualou, lililojengwa Mwaka 1907, liliwahi kutumika kuwa kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kuhifadhi umeme, capacitor baada ya miaka ya 1960 ya karne ya 20. Mwaka 1983, Kamati ya Chama ya Mji wa Xiamen na Serikali ya mji huo ziliamua kujenga jumba la makumbusho hapa.
Wakati huo, Xiamen ilihitaji maendeleo kila mahali na ilikuwa na upungufu wa fedha kila mahali. Ili kufanya ukarabati wa Jengo la Bagualou, bajeti ya awali punde haikutosha.
Mwaka 1986, Xi Jinping, wakati huo akiwa mjumbe wa kudumu wa Kamati ya Chama ya Mji wa Xiamen na naibu meya wa mji huo, aliidhinisha kutenga yuan 300,000 baada ya kukagua Jengo la Bagualou, na kutatua hitaji la haraka la kazi ya ukarabati. Kwa uungaji mkono wa fedha hizo, Jengo la Bagualou lilikarabatiwa upya.
Tangu Mwaka 2005, jengo kuu la Bagualou limefunguliwa kwa nje, likiitwa Jumba la Makumbusho la Gulangyu Organ, na linapokea watalii wastani wa zaidi ya 500,000 kila mwaka.
Julai 8, 2017, "Kisiwa cha Gulangyu: Eneo la Makazi ya Kimataifa ya Kihistoria" kiliorodheshwa kwa mafanikio kwenye Orodha ya Mali ya Urithi wa Dunia. Miongoni mwake, Jengo la Bagualou, likiwa moja ya sehemu kuu za Mali ya Urithi wa Kitamaduni wa Dunia wa Gulangyu, limesifiwa sana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Mali ya Urithi wa Dunia.
Huku akifurahia kusikia kwamba Kisiwa cha Gulangyu kimeorodheshwa kwa mafanikio kuwa Mali ya Urithi wa Dunia, Xi Jinping alitoa maagizo muhimu: Madhumuni ya kutoa ombi la kuorodheshwa kuwa Mali ya Urithi wa Dunia ni kukilinda na kukitumia vizuri zaidi . Ni muhimu kufanya majumuisho ya uzoefu uliofanikiwa, kujifunza kutoka kwa dhana za kimataifa, na kukamilisha mfumo wa muda mrefu, kulinda kwa uangalifu mali ya urithi wa kitamaduni iliyoachwa na mababu zetu, na kuwezesha muktadha wa kihistoria kurithishwa vyema kwa vizazi.
Kisiwa cha Gulangyu kinajulikana kuwa ni "Makumbusho ya Majengo ya Mataifa Yote". Likiwa ni eneo la kitaifa la ulinzi wa mabaki ya kitamaduni, Jengo la Bagualou ni moja ya mambo ya msingi ya mali ya urithi wa kitamaduni wa dunia wa Kisiwa cha Gulangyu. (Picha na Yang Jinjian)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma