超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Xi Jinping asisitiza kukamilisha mfumo wa viwanda vya kisasa wenye umaalum wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 12, 2024

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) siku ya Jumanne alipokuwa akiongoza mkutano wa tano wa kamati kuu ya kuendeleza kwa kina mageuzi, amesisitiza juhudi za kukamilisha mfumo wa viwanda vya kisasa wenye umaalum wa China, na kujenga mazingira ya kufungua mlango ya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia yenye nguvu ya kufanya ushindani duniani.

Mkutano huo umejadili na kupitisha miongozo ya kukamilisha utaratibu wa viwanda vya kisasa wenye umaalum wa China, kukamilisha mfumo wa kuhakikisha mapato na maslahi ya wakulima wanaolima na kuzalisha nafaka, na kukamilisha mfumo wa kutoa ruzuku na fidia kwenye maeneo makuu yanayozalisha nafaka, na kujenga mazingira ya kufungua mlango ya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia yenye nguvu ya kufanya ushindani duniani.

Rais Xi amesisitiza kuimarisha uongozi wa Chama, kukamilisha mfumo wa usimamizi wa kampuni, kuhimiza viwanda vya kiserikali vitekeleze kwa umakini majukumu yao.

Amesema, ni lazima kuhamasisha wakulima kulima nafaka na kuchochea juhudi za serikali za mitaa katika kuongeza uzalishaji wa nafaka ili kuhakikisha usalama wa chakula.

Rais Xi amesema, ni muhimu pia kuchochea uvumbuzi kwa kupitia kufungua mlango, huku akitoa wito wa ufunguaji mlango kwenye sekta ya teknolojia, kujenga mfumo wa uvumbuzi wa kuelekea dunia nzima, na kushiriki kwa juhudi kwenye uvumbuzi wa dunia nzima.

Ili kukamilisha utaratibu wa kampuni za kisasa, ni lazima kuheshimu viwanda vikiwa wadau wakuu katika shughuli za uendeshaji, kukamilisha usimamizi wa kisasa wa viwanda vya kiserikali, na kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa mali ya kitaifa, mkutano huo umesema.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Li Qiang, Wang Huning na Cai Qi, ambao wote ni wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na manaibu wakurugenzi wa kamati kuu ya kuendeleza kwa kina mageuzi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha