Lugha Nyingine
Kuwekeza Xinjiang, China: Kampuni za kigeni zimevutiwa na mambo gani huko Xinjiang?
Mkuu wa Kampuni ya Mauzo ya Chakula ya Slavs tawi la Urumqi Krasik Pavel akiuliza sera kuhusu biashara kwenye Kituo cha Huduma kwa Kampuni za Kigeni cha Eneo la Maendeleo ya Uchumi na Teknolojia la Urumqi. (Picha na Han Ting/People’s Daily Online)
“Kuna fursa nyingi hapa Xinjiang, zikisubiria wawekezaji mwafaka kuzigundua,” anasema Hendrik Sybrand Alblas, mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Kimataifa ya Usafirishaji ya Alblas ya Uholanzi.
Fursa zipo wapi? Kwa kuingia Eneo la Maendeleo ya Uchumi na Teknolojia la Urumqi (linajulikana pia kama eneo la Toutunhe), jibu linaweza kupatikana kutoka kampuni mbili za kigeni.
Yakiwa yamebeba bidhaa za PVC, sehemu za magari na bidhaa nyingine mbalimbali kutoka kwenye karakana, malori ya kampuni ya Alblas tawi la Xinjiang, taratibu huendeshwa kutoka Eneo la Bandari ya Kimataifa ya Nchi kavu la Urumqi na kuzipeleka Ulaya. Mwaka 2009 kampuni hiyo ilihamisha makao yake makuu ya China kutoka Shanghai mpaka Urumqi, Xinjiang, ikiona fursa za sera ya China ya kuendeleza eneo la Magharibi na faida za kijiografia za Xinjiang kuwa “njia ya dhahabu” kati ya Asia na Ulaya.
Kampuni nyingine ya kigeni ambayo pia inathamini faida bora za kijiografia za Xinjiang ni Kampuni ya Mauzo ya Chakula ya Slavs tawi la Urumqi. Mkuu wa kampuni hiyo Krasik Pavel amesema kuwa, “Xinjiang inapakana na Kazakhstan, ambayo ni faida kifursa. Chakula cha kuganda tunachouza China husafirishwa kutoka Belarus, kinapita Kazakhstan, kuidhinishwa na forodha za Xinjiang, China na hupelekwa kwa washirika katika miji mbalimbali nchini China.
Mwezi Januari mwaka huu, chini ya usaidizi wa Kampuni ya Kuwasaidia Wajasirimali wa Xinjiang na Asia ya Kati, kampuni ya Pavel ilisajiliwa kwa mafanikio katika Eneo la Majaribio la Biashara Huria la Xinjiang huko Urumqi. Kuanzia kazi ya ukalimani, usajili wa forodha hadi majadiliano kuhusu usafirishaji, kampuni hiyo ya msaada wa wajasirimali kwenye Kituo cha Huduma kwa Kampuni za Kigeni imekuwa ikitatua vizuri changamoto mbalimbali za kampuni za kigeni zilizowekeza Xinjiang, ikifanya kazi kama daraja kati ya kampuni na serikali. Hadi sasa imesaidia kwa mafanikio kampuni 14 za kigeni kuingia kwenye Eneo la Majaribio la Biashara Huria la Xinjiang huko Urumqi.
Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na kuzidisha ufunguaji mlango wa China kwa Magharibi na ujenzi wa eneo la msingi na kiini la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, Xinjiang imekuwa lango muhimu la ufunguaji mlango wa China kwa Magharibi.
Kwa Eneo la Majaribio la Biashara Huria la Xinjiang, ambalo lilizinduliwa Novemba mwaka jana, Dilixiati Maimaiti, mwakilishi mkuu wa kampuni ya Alblas tawi la China amejawa na matarajio sana juu yake. “Sera za upendeleo za eneo hilo la majaribio la biashara huria zitavutia bidhaa nyingi zaidi za kuuzwa na kuagizwa nje ya China kukusanyika hapa, ikitoa vyanzo zaidi vya bidhaa kwa ajili ya usafirishaji wa barabara” amesema.
Lori la Kampuni ya Alblas likitoka Eneo la Bandari ya Kimataifa ya Nchi kavu la Urumqi. (Picha na Han Ting/People’s Daily)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma