Lugha Nyingine
Xi Jinping atuma salamu za pongezi kwa miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Kijeshi cha Huangpu
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ametuma salamu za pongezi kwa jumuiya ya wahitimu wa Chuo cha Kijeshi cha Huangpu kwa maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho na maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa jumuiya ya wahitimu wa chuo hicho.
Kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Rais Xi ametoa salamu za pongezi kwa jumuiya ya wahitimu wa chuo hicho na salamu za dhati kwa wahimitimu hao na jamaa zao walioko ndani na nje ya China.
Chuo cha Kijeshi cha Huangpu (Whampoa), kilichoanzishwa kutokana na ushirikiano wa kwanza kati ya Chama cha Kuomintang cha China (KMT) na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), kilisimama kama chuo cha kwanza cha kuandaa na kuendeleza maofisa wa kijeshi kwa mapinduzi ya China, Rais Xi amesema katika barua hiyo.
Jumuiya ya wahitimu wa chuo hicho, ambayo ni jumuiya ya wazalendo chini ya uongozi wa CPC inayowashirikisha wahitimu wa chuo hicho na jamaa zao ndani na nje ya China, imechangia katika maendeleo ya jumla ya Chama na nchi na imefanya juhudi kubwa katika kupanua mawasilianio na ushirikiano kati ya pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan, kupinga shughuli za wafarakanishaji wa kuifanya “Taiwan ijitenge” na kuhimiza Muungano wa Taifa.
Ameelezea matumaini yake kwamba wahitimu hao na jamaa zao wa ndani na nje ya China watashiriki kikamilifu katika ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na kuchangia katika ujenzi wa nchi yenye nguvu na kufikia ustawishaji wa kitaifa.
Chuo cha kijeshi cha Huangpu kilianzishwa huko Guangzhou, Kusini mwa China Juni 1924.
Kongamano hilo la kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Kijeshi cha Huangpu na maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wahitimu wa chuo hicho limefanyika Beijing siku ya Jumatatu. Ujumbe huo wa Rais Xi ulisomwa kwenye kongamano hilo.
Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, alihudhuria kongamano hilo na kutoa hotuba.
Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, akihudhuria kongamano la kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Kijeshi cha Huangpu na maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wahitimu wa chuo hicho na kutoa hotuba kwenye kongamano hilo mjini Beijing, China, Juni 17, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)
Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, akihudhuria kongamano la kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Kijeshi cha Huangpu na maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wahitimu wachuo hicho na kutoa hotuba kwenye kongamano hilo mjini Beijing, China, Juni 17, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)
Wang Huning, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, akihudhuria kongamano la kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Kijeshi cha Huangpu na maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wahitimu wa chuo hicho na kutoa hotuba kwenye koongamano hilo mjini Beijing, China, Juni 17, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma