Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa maagizo muhimu kuhusu kupambana na mafuriko na hali ya ukame
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa maagizo muhimu juu ya kazi ya kupambana na mafuriko na hali ya ukame.
Rais Xi amedhihirisha kuwa mvua kubwa imeendelea kunyesha katika maeneo mengi ya kusini mwa China, na mafuriko na majanga ya kijiolojia yametokea katika mikoa ya Guangdong na Fujian pamoja na mikoa mingine, na kusababisha madhara kwa binadamu na hasara ya mali. Amesema katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa China, hali ya ukame imetokea na kuenea kwa kasi. Ni wazi kuwa mafuriko kusini na hali ya ukame kaskazini nchini China.
Ametoa wito wa kufanya juhudi kwa nguvu zote katika kukabiliana na maafa, kufanya kila linalowezekana kutafuta na kuokoa wale wasiojulikana walipo, na kuwapanga vizuri waathirika wa janga hilo, kuhakikisha utaratibu wa kawaida wa uzalishaji na maisha, na kupunguza hasara.
Rais Xi amesisitiza kuwa wakati ambapo China inaingia katika msimu wa mafuriko, hali ya kupambana na mafuriko inazidi kuwa ngumu, hivyo mikoa yote na idara husika zinatakiwa kuongeza uelewa juu ya hatari, kujiandaa kwa uwezekano wa kukabiliana na hali mbaya zaidi, kuwafanya wale wanaosimamia watekeleze wajibu wao kwa umakini zaidi, na kuimarisha uratibu na upangaji mipango, ili kuhakikisha kazi mbalimbali zinafanyika bila kulegalega hata kidogo katika kupambana na mafuriko na hali ya ukame, kuwaokoa na kuwasaidia watu wanaokumbwa na maafa na kupunguza hasara.
Rais Xi pia amehimiza juhudi za kuimarisha ufuatiliaji na tahadhari za mapema za majanga, kudhibiti hatari kwa wakati, kuandaa mahitaji na vifaa vya kutosha, na mipango bora ya kazi, ili kukabiliana ipasavyo na kwa ufanisi matukio ya dharura, na kulinda maisha ya watu na mali zao pamoja na utulivu wa mambo makuu ya kijamii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma