Lugha Nyingine
Kamati Kuu ya CPC kufanya mkutano wa wajumbe wote kuhusu mageuzi kuanzia Julai 15 hadi 18
BEIJING - Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kitafanya mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 kuanzia Julai 15 hadi 18 mjini Beijing, ambao utajadili hasa masuala kuhusu kuendeleza zaidi mageuzi kwa kina na kwa pande zote na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC umesema siku ya Alhamisi.
Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, ameongoza mkutano huo wa Alhamisi.
Mkutano huo umeamua kuwasilisha mswada wa uamuzi juu ya kuendelelza zaidi mageuzi kwa kina na kwa pande zote na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China kwenye mkutano huo wa wajumbe wote wa kamati kuu ya CPC ili kujadiliwa na kupitishwa.
Kwenye mkutano huo wa Alhamisi, wajumbe wa Ofisi ya Siasa walisikiliza maoni kuhusu mswada huo ambayo yalikusanywa kutoka ndani na nje ya Chama. Mswada huo utarekebishwa upya baada ya majadiliano kwenye mkutano huo.
Mkutano huo umeeleza kuwa, mswada huo umechambua kwa kina hali mpya na matatizo mapya katika kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na kupanga mpango wa jumla kwa njia ya kisayansi kuhusu kuendeleza zaidi mageuzi kwa kina na kwa pande zote.
Mkutano huo umedhihirisha kwamba, mswada huo ni waraka wa mwongozo unaoongoza kuendeleza mageuzi kwa kina na kwa pande zote katika safari mpya na inaonyesha dhamiria ya Kamati Kuu ya CPC na Xi akiwa katibu mkuu wake, ya kufungua matarajio mapana ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China kwa kupitia kuendeleza zaidi mageuzi kwa kina.
Mkutano huo ukifafanua kuhusu malengo na madhumuni ya kuendeleza zaidi mageuzi, umesema China itakamilisha ujenzi wa uchumi wa soko huria wa kijamaa kwa vigezo vya juu ifikapo Mwaka 2035.
Mfumo wa utawala na uwezo wa utawala kimsingi utafanywa kuwa wenye mambo ya kisasa na ujenzi wa mambo ya kisasa ya kijamaa utatimizwa kimsingi ifikapo Mwaka 2035, mkutano huo umeongeza.
Mkutano huo umeainisha kanuni zinazopaswa kufuatwa katika kuendeleza mageuzi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma