Lugha Nyingine
Rais Xi atunuku bendera ya heshima kwa brigedi ya askari wa mizinga ya PLA
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitunuku bendera ya heshima kwa Brigedi ya askari wa mizinga ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), ambayo imepata tuzo ya heshima ya " Brigedi ya Mfano wa Kuigwa ya Askari wa Mizinga" na wakipiga picha na wajumbe wa brigedi iliyotunukiwa kwenye hafla iliyoandaliwa na CMC mjini Beijing, China, Julai 9, 2024. (Xinhua/Li Gang)
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), Jumanne kwenye hafla iliyoandaliwa na CMC mjini Beijing ametunuku bendera ya heshima kwa brigedi ya askari wa mizinga ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), ambayo imetunukiwa tuzo ya heshima ya "Brigedi ya Mfano wa Kuigwa ya Askari wa Mizinga".
Wajumbe wa brigedi hiyo walimpigia saluti Rais Xi kabla ya kupokea bendera. Rais Xi ametoa pongezi zake.
Kwenye hafla hiyo, Zhang Youxia, naibu mwenyekiti wa CMC, alisoma amri ya kutunuku tuzo hiyo ya heshima iliyotiwa saini na Rais Xi. He Weidong, naibu mwenyekiti mwingine wa CMC, aliongoza hafla hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma