Lugha Nyingine
Kampuni ya China yasaidia kubadilisha sekta ya ujenzi ya Kenya kupitia teknolojia ya kutengeneza tayari mapema sehemu za majengo
Picha iliyopigwa Mei 17, 2024 ikionesha Kampuni ya kutengeneza mapema sehemu tayari za jengo ya China Wu Yi Tawi la Kenya katika mji wa viwanda wa Mto Athi, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)
NAIROBI – Umbali wa takriban kilomita 30 kusini-mashariki ya Nairobi, mji mkuu wa Kenya, kampuni ya kutengeneza mapema sehemu tayari za jengo ya China Wu Yi Tawi la Kenya imejenga kiwanda kikubwa cha teknolojia mpya za ujenzi, kikisababisha mabadiliko makubwa katika sekta ya ujenzi nchini humo.
Mnamo mwaka 2016, kampuni hiyo ilianzisha Kituo cha Utafiti, Maendeleo na Uzalishaji wa Mambo ya Ujenzi cha Kenya pamoja na mradi wa soko la nyenzo za ujenzi linaloitwa "Kiwanda cha Wu Yi " katika mji wa viwanda wa Mto Athi.
Kiwanda cha Wu Yi ni maajabu ya kiusanifu yaliyopo kati ya uwanda tulivu na mashamba. Kwa miaka kadhaa iliyopita, kiwanda hicho kimekuwa kikitoa sehemu za jengo zilizotengenezwa tayari mapema, ikiwa ni pamoja na mbao wa zege, mihimili ya chuma, na nguzo, kwa ajili ya kuunganisha sehemu zake na kuunda nyumba ya kisasa.
Ndani ya eneo hilo kubwa linalojumuisha kiwanda cha uzalishaji, soko la nyenzo za ujenzi, na eneo la makazi, vijana wenyeji kama Brian Calisto Kariuki wamepata ajira yenye manufaa, jukwaa la kujipatia undani juu ya teknolojia ya ujenzi wa kutengeneza tayari mapema sehemu za jengo.
Akiwa ni mhandisi wa kijiografia, kijana huyu mwenye umri wa miaka 30, alijiunga na Kampuni hiyo ya China Wu Yi mwaka 2017 kufanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza tayari mapema sehemu za jengo na amekuwa akipanda vyeo vyake hadi kuwa meneja msaidizi wa kampuni hiyo.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na shirika la habari la China Xinhua, Kariuki amebainisha kuwa, kwa teknolojia hiyo ya kutengeneza tayari mapema sehemu za jengo kupatikana kwa urahisi, mjenzi anatakiwa tu kuunganisha sehemu hizo tayari za nguzo na mbao kwenye eneo la ujenzi; teknolojia hii inapunguza muda wa ujenzi na kudumisha ubora mzuri.
"Ukitumia nyenzo zilizotengenezwa tayari mapema, unaweza kumaliza ghorofa nne ndani ya mwezi. Kwa hivyo unaokoa muda na pesa. Unaweza kudhibiti ubora wa zege," amesema Kariuki.
Hadi sasa, kampuni hiyo ya Wu Yi ya China imejenga majengo alama kwa kutumia teknolojia hiyo, ikiwa ni pamoja na majengo ya pensheni ya Benki Kuu ya Kenya na jengo la maduka la Rose Avenue huko Nairobi, amesema Kariuki.
Picha iliyopigwa Mei 17, 2024 ikionesha mwonekano wa nje wa Jengo la Maduka la Coloho katika mji wa viwanda wa Mto Athir, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)
Mfanyakazi akifanya kwenye karakana ya Kampuni ya China Wu Yi (Kenya) katika mji wa viwanda wa Mto Athi, Kenya Mei 17, 2024. (Xinhua/Li Yahui)
Picha iliyopigwa Mei 17, 2024 ikionesha muonekano wa ndani wa Jengo la Maduka la Coloho katika mji wa viwanda wa Mto Athi, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma