Lugha Nyingine
Mnyanyua vyuma?wa China apata?medali ya dhahabu ya Olimpiki, timu ya kuogelea kwa mtindo wa sarakasi?ya China yaweka historia
Li Fabin wa China akishindana kwenye mchezo wa kunyanyua uzani kwa wanaume wenye uzito wa kilo 61 kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris Agosti 7, 2024. (Xinhua/Yang Lei)
PARIS – Wachezaji wa kunyanyua vyuma wa China Li Fabin na Hou Zhihui, ambao wote ni mabingwa watetezi wa Michezo ya Olimpiki, wamehifadhi mataji yao kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, huku China pia ikinyakua medali yake ya kwanza kabisa ya dhahabu katika mchezo wa kuogelea kwa mtindo wa sarakasi siku ya Jumatano.
Baada ya Siku ya 12, Marekani inaongoza kwa idadi ya medali ikiwa na medali za dhahabu 27, huku China ikiendelea kuwa katika nafasi ya pili kwa medali 25 za dhahabu.
Li mwenye umri wa miaka 31 ameweka rekodi ya Olimpiki ya kunyanyua vyuma vya uzito wa kilo 143 katika hatua ya kuchukua na kunyanyua juu kwa haraka, na kunyanyua vyuma vya uzito wa kilo 167 katika hatua ya kuchukua na kunyanyua juu kwa taratibu, akiwa na jumla ya uzani wa kilo 310 kutetea taji lake la Olimpiki kwenye mchezo huo wa kunyanyua vyuma kwa wanaume wenye uzito wa kilo 61 katika shughuli ya kwanza ya kunyanyua vyuma ya michezo hiyo ya Olimpiki.
Hou Zhihui wa China akishangilia baada ya kushinda mchezo wa kunyanyua uzani kwa wanawake wenye uzito wa kilo 49 kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris Agosti 7, 2024. (Xinhua/Fei Maohua)
China imehifadhi medali nyingine ya dhahabu ya kunyanyua vyuma saa chache baadaye wakati Hou Zhihui aliposhinda katika mchezo wa kunyanyua vyuma kwa wanawake wenye uzito wa kilo 49. Bingwa huyo mtetezi mwenye umri wa miaka 27 alinyanyua kilo 89 katika hatua ya kuchukua na kunyanyua juu kwa haraka, na kuweka rekodi ya Olimpiki katika hatua ya kuchukua na kunyanyua juu kwa taratibu kwa kunyanyua kilo 117 kwa jumla ya kilo 206, akimshinda kwa manusura mshindi wa medali ya fedha Mihaela Cambei wa Romania kwa kilo 1.
Katika wakati wa kihistoria kwa China, imepata medali yake ya kwanza ya dhahabu ya Olimpiki katika mchezo wa kuogelea kwa mtindo wa sarakasi. Ikiongoza kutoka kwenye raundi mbili za kwanza katika kipengele cha timu, China ilitawala katika raundi ya sarakasi ya kawaida kwa pointi 283.6934, ikimaliza na jumla ya pointi 996.1389 na kushinda medali ya dhahabu.
Timu ya China ikishindana kwenye mchezo wa kuogelea kwa mtindo wa sarakasi kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris, Agosti 7, 2024. (Xinhua/Xia Yifang)
"Ni heshima kubwa kwamba tumechukua utukufu wa Olimpiki kwa mara ya kwanza. Imekuwa heshima kubwa kuweka historia kwa nchi yetu," kocha mkuu wa China Zhang Xiaohuan amesema.
Alvaro Martin (Kulia) na Maria Perez wa Hispania wakishangilia baada ya mbio za kutembea kwa kasi za marathon kwa wanawake na wanaume kupokezana katika Michezo ya Olimpiki ya Paris Agosti 7, 2024. (Xinhua/Li Gang)
Katika mechi ya kwanza kabisa kwa mbio za marathon za kutembea kwa kasi kwa wanawake na wanaume kupokezana katika Olimpiki, Alvaro Martin na Maria Perez wamejishindia medali ya kwanza ya dhahabu ya riadha ya Hispania huko Paris kwa kushinda mbio hizo kwa kutumia saa mbili na dakika 50.31, mbele ya Brian Pintado na Glenda Morejon wa Ecuador, ambao wametwaa medali ya fedha kwa kutumia muda wa 2: 51:22.
Guo Qing (Kulia) wa China akijibu mapigo katika fainali ya taekwondo ya wanawake kwa wachezaji wenye uzito wa kilo 49 dhidi ya Panipak Wongpattanakit wa Thailand kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris Agosti 7, 2024. (Xinhua/Li Ying)
Medali ya kwanza ya dhahabu ya mchezo wa taekwondo katika Michezo hiyo imeenda kwa Panipak Wongpattanakit wa Thailand, wakati bingwa huyo mtetezi katika kipengele cha wachezaji wenye uzito wa kilo 49 kwa wanawake alipomshinda Guo Qing wa China katika fainali kwa 2-1.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma