Lugha Nyingine
WHO yaitisha kamati ya dharura kwa ajili ya kukabiliana na kuenea kwa mpox
(CRI Online) Agosti 08, 2024
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, WHO inaitisha kamati ya dharura kwa ajili ya kukabiliana na kuenea kwa mpox nje ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na uwezekano wa kuenea zaidi duniani.
Akiongea na wanahabari Jumatano mjini Geneva Tedros amesema, kamati hiyo itakutana “haraka iwezekanavyo” ili kutathmini kama mlipuko wa maradhi hayo utakuwa tukio la dharura ya afya ya umma inayohitaji ufuatiliaji kote duniani.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma