超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Shule saba za Uganda zafungwa katika eneo la magharibi wakati ambapo mafuriko yameanza

(CRI Online) Agosti 08, 2024

Mamlaka ya Uganda imesema takriban shule saba za msingi na sekondari zimefungwa katika wilaya ya magharibi ya Ntoroko kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Akizungumza kwa njia ya simu na Shirika la Habari la China, Xinhua mkuu wa wilaya ya Ntoroko, Edward Bashungura, amesema mvua hiyo kubwa imesababisha Mto Semliki na Ziwa Albert lililopo karibu kufurika kingo, na kusababisha mafuriko, ambapo vijiji 20 vimeathiriwa na shule nyingi kuzama.

Bashungura ameongeza kuwa hawakuwa na namna ila kufunga shule hizo kwa ajili ya usalama wa watoto, huku shule nyingi zaidi zikifanyiwa tathmini na kutakiwa kufungwa.

Afisa huyo amesema katika vijiji hivyo pekee, watu 20,000 wameathiriwa na mafuriko. Amebainisha kuwa wanachohitaji sasa ni kurejesha madaraja yaliyosombwa na maji, mahema kwa ajili ya shule, makazi ya wanakijiji walioathirika na vifaa vya kusafisha chakula na maji.

Wiki iliyopita, mamlaka ya hali ya hewa ya nchi hiyo ilitangaza kuwa nchi hiyo itakabiliwa na mvua kubwa na radi mwanzoni mwa Agosti.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha