Lugha Nyingine
Afrika CDC yataka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya kuenea kwa mpox
(CRI Online) Agosti 09, 2024
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kuepusha kuenea kwa mpox katika bara zima.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuhusu mlipuko wa mpox unaoenea katika nchi nyingi barani Afrika, Mkurugenzi Mkuu wa CDC barani Afrika Jean Kaseya amesema nchi zaidi ya 16 katika kanda zote tano za Afrika zimeathiriwa na mpox.
Amesema kuwa wagonjwa takriban 38,465 na vifo 1,456 vimeripotiwa barani Afrika kuanzia mwezi Januari mwaka 2022, wakiwemo wagonjwa 887 na vifo vitano katika wiki iliyopita.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma