Lugha Nyingine
Waziri wa Uganda apongeza juhudi za China katika kulinda mazingira
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uganda Victoria Rusoke Businge amepongeza mchango wa serikali ya China na shirika lisilo la kiserikali la China katika kulinda mazingira na kurejesha misitu nchini Uganda.
Businge aliyasema hayo Jumatano mjini Kampala, wakati akilikabidhi Shirika la Mamlaka ya Kanda ya Ziwa Victoria (LVRLAC) miti na miche ya matunda elfu kumi iliyotolewa na Shirika Liliso la Kiserikali la Mfuko wa Kuokoa Wanyama na Mimea (SWF).
Pia amesisitiza ushirikiano wa muda mrefu kati ya serikali za miji, ikiwa ni pamoja na mji wa Entebbe nchini Uganda, na mji wa Wuhan nchini China kwenye sekta za ujenzi wa miundombinu na uungaji mkono wa mazingira.
Konsuli wa uchumi na biashara katika ubalozi wa wa China nchini Uganda Wang Jianxun amesema China imeanza safari mpya ya kujenga nchi ya ujamaa yenye mambo ya kisasa, ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa mazingira, na kuhamasisha kampuni nyingi zaidi za China kushiriki kwenye programu za uhifadhi wa mazingira na majukumu ya kijamii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma