超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Msemaji wa Mambo?ya Nje wa China?ajibu swali?kuhusu wanajeshi wa Ukraine kuvuka na kuingia Russia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 13, 2024

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China siku ya Jumatatu alisema msimamo wa China kuhusu suala la Ukraine ni wa siku zote na wazi.

Imekuwa ikiripotiwa kuwa hivi karibuni askari wa Ukraine walianzisha mashambulizi katika eneo la Russia la mkoa wa Kursk. Russia imesema kuwa mashambulizi hayo ya jeshi la Ukraine yamesababisha vifo vya raia zaidi ya 60, na jeshi la Russia limezuia mashambulizi hayo ya jeshi la Ukraine. Mkoa wa Kursk umetangaza hali ya hatari.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema katika hotuba yake kwamba Russia ilileta vita katika nchi yake Ukraine, na sasa Russia hakika imehisi matokeo yake.

Upande wa Marekani umesema haukufahamishwa kabla ya mashambulizi hayo, kwamba upande wa Marekani hauhisi kama jambo hilo ni kuchochea zaidi hali ya mgogoro huo kwa njia yoyote na kwamba Ukraine inafanya kile inachohitaji kufanya ili kufanikiwa kwenye uwanja wa vita. Upande huo wa Marekani umesema kuwa mashambulizi hayo yanaendana na sera ya Marekani kuhusu kile Ukraine inaweza na haiwezi kufanya kwa kutumia silaha za Marekani, kwamba Marekani inaiunga mkono Ukraine kujilinda dhidi ya mashambulizi yanayovuka mpaka.

Alipotakiwa kuzungumzia maendeleo ya hali ya mambo, msemaji huyo amesema upande wa China unatoa wito kwa pande zote kufuata kanuni tatu za kupunguza hali ya wasiwasi ya mgogoro huo, kanuni ambazo ni kutopanua uwanja wa vita, kutopamba moto kwa mapigano na kutouacha upande wowote kuchochea moto wa vita.

China itaendelea kudumisha mawasiliano na jumuiya ya kimataifa ili kufanya kazi yake ya kiujenzi kwa ajili ya utatuzi wa kisiasa wa mgogoro huo, amesema msemaji huyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha