Lugha Nyingine
China yasema maendeleo endelevu ni msingi wa amani ya kudumu barani Afrika
Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong amesema, kazi ya msingi katika kukabiliana na historia ya udhalimu barani Afrika ni kuziunga mkono nchi za Afrika katika njia ya maendeleo endelevu kama msingi wa amani ya kudumu.
Balozi Fu amesema hayo katika mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika jana kuhusu “Kushughulikia Historia ya Udhalimu na Kuimarisha Uwakilishi Madhubuti wa Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.”
Balozi Fu amesema ili kuondokana na ukosefu wa usawa kwa bara la Afrika, jamii ya kimataifa inapaswa kupinga bila kusita urithi wa ukoloni na aina zote za vitendo vya kidhalimu, na nchi za Magharibi zinapaswa kubeba wajibu wao kihalisi wa kihistoria, kubadili mwelekeo wao, kuacha kuingilia mambo ya ndani ya nchi hizo na kurejesha mustakabali wa siku za baadaye wa Afrika kwa Waafrika wenyewe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma