Lugha Nyingine
Mahakama nchini Kenya yazima mgomo wa walimu
(CRI Online) Agosti 29, 2024
Mahakama ya Kazi jijini Nairobi nchini Kenya imesitisha mgomo wa walimu unaoendelea ulioitishwa na Chama cha Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya mafunzo (KUPPET).
Akitoa agizo hilo jana, Jaji James Rika amesema mgomo huo unasimamishwa hadi kesi iliyowasilishwa na Tume ya Huduma ya Walimu (TSC) itakaposikizwa na kutolewa hukumu. Kesi hiyo itatajwa Septemba 5, 2024.
Walimu hao walianza mgomo wao Jumatatu wiki hii na kufanya maandamano katika maeneo mbalimbali nchini humo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma