Lugha Nyingine
Makamu Rais wa China Han Zheng akutana na Rais Vladimir Putin wa Russia
Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Rais Vladimir Putin wa Russia mjini Vladivostok, Russia, Septemba 4, 2024. (Xinhua/Wang Ye)
VLADIVOSTOK - Makamu Rais wa China Han Zheng amekutana na Rais Vladimir Putin wa Russia mjini Vladivostok, mji wa Mashariki ya Mbali nchini Russia siku ya Jumatano ambapo amewasilisha salamu za Rais Xi Jinping wa China kwa Putin
Amesema kuwa katika hatua hii mpya ya kihistoria ya maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano kati ya pande mbili, uhusiano kati ya China na Russia katika zama mpya unaendelea kwa kiwango cha juu chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili.
Han amesema China ina imani kubwa katika mustakabali wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Ameeleza kuwa China inathamini sana mchango na ushawishi wa Baraza la Uchumi la Mashariki, inaunga mkono na kushiriki kikamilifu katika maendeleo na ushirikiano wa eneo la Mashariki ya Mbali la Russia, na inapenda kunufaisha fursa za maendeleo na Russia, ili kunufaisha watu wa pande zote mbili kwa mafanikio zaidi na kuhimiza maendeleo na ustawishaji wa pamoja.
Kwa upande wake Putin amemkaribisha Han nchini Russia kushiriki Baraza la tisa la Uchumi la Mashariki na kumwomba kufikisha salamu zake za kirafiki na za kutakia kila la kheri kwa Rais Xi.
Akisema kuwa uhusiano kati ya Russia na China uko katika kipindi bora zaidi katika historia, Rais Putin amesema Russia inathamini sana ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali kama vile uchumi, biashara, utamaduni na mawasiliano kati ya serikali za mitaa na wadau wa pande zote mbili na inatazamia kupata fursa mpya zaidi za maendeleo na China.?
Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Rais Vladimir Putin wa Russia mjini Vladivostok, Russia, Septemba 4, 2024. (Xinhua/Wang Ye)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma