Lugha Nyingine
Rais wa China atuma pongezi kwa kiongozi wa DPRK?kwa kuadhimisha Miaka 76 tangu kuanzishwa kwa nchi yake
Rais Xi Jinping wa China amemtumia salamu za pongezi kiongozi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) Bw. Kim Jong Un kutokana na Maadhimisho ya Miaka 76 tangu kuanzishwa kwa nchi yake.
Katika salamu hizo, Rais Xi ameeleza kuwa, anaamini chini ya uongozi wa chama tawala cha Wafanyakazi kinachoongozwa na Bw. Kim Jong Un, watu wa DPRK watapata mafanikio makubwa zaidi katika mchakato wa kuhimiza mambo ya ujamaa wenye umaalumu wa Korea Kaskazini.
Rais Xi pia amesisitiza kuwa, kutokana na hali mpya katika zama mpya, China itaendelea kuuchukulia uhusiano kati yake na DPRK kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na ina nia ya kukuza mawasiliano ya kimkakati, kuimarisha uratibu na ushirikiano na DPRK, kulinda, kuimarisha na kuendeleza uhusiano na ushirikiano na urafiki wa jadi kati ya pande hizo mbili, kuhimiza kwa pamoja mambo ya ujamaa, ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuhimiza amani na utulivu, na maendeleo na ustawi wa kikanda na wa dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma