Lugha Nyingine
Mivutano ya siasa?za?kijiografia, mapinduzi ya kidijitali, mabadiliko ya tabianchi vimebadilisha muundo wa?maendeleo: WTO
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Ngozi Okonjo-Iweala akitoa hotuba mkutano wa 12 kuhusu Mradi wa China wa WTO yaliyofanyika Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu, Februari 25, 2024. (WTO/kupitia Xinhua)
GENEVA – Mienendo inayoibuka ya kimataifa kama vile mivutano ya siasa za kijiografia, mapinduzi ya kidijitali na mabadiliko ya tabianchi vimebadilisha muundo wa maendeleo yanayoongozwa na biashara, Shirika la Biashara Duniani (WTO) limesema katika ripoti kuu iliyotolewa jana siku ya Jumatatu.
Katika toleo la 2024 la "Ripoti ya Biashara Duniani," WTO imekadiria kuwa mambo ya kimataifa kama vile mivutano ya siasa za kijiografia, migogoro ya kikanda na vikwazo vya biashara vimeathiri msingi thabiti wa ukuaji wa uchumi wa dunia katika miaka 30 iliyopita, vikiwa na uwezekano wa kusababisha mgawanyiko wa kibiashara.
Kwa upande mwingine, kuongezeka kwa msukumo wa mtaji na ujuzi wa viwanda vya kisasa kumepunguza wigo wa ukuaji unaoongozwa na viwanda katika nchi zenye uchumi wa kipato cha chini. Wakati huo huo, mabadiliko ya tabianchi yanaleta changamoto kubwa zaidi, haswa kwa nchi hizo.
Hata hivyo, ripoti hiyo pia imesisitiza fursa mpya zinazoletwa na mwelekeo huu wa kimataifa. Kwa mfano, nchi zinazoendelea kiuchumi zinaweza kupunguza gharama za biashara kupitia matumizi ya teknolojia za kidijitali, kugeukia ukuaji unaoongozwa na uchumi wa huduma, au kuchukua fursa za mahitaji ya rasilimali mpya katika mageuzi ya kijani duniani ili kupata maendeleo.
Ripoti hiyo imewasilisha ushahidi thabiti kwamba biashara imekuwa na mchango mkubwa katika kupunguza tofauti za kipato kati ya makundi mbalimbali ya uchumi tangu WTO ilipoanzishwa miaka 30 iliyopita.
"Pengine jambo kubwa zaidi la kuchukua kutoka kwenye ripoti hiyo ni kutambua tena mchango wa kimageuzi wa biashara katika kupunguza umaskini na kuleta ustawi wa pamoja," Mkurugenzi Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala amesema katika dibaji yake ya ripoti hiyo.
William Widjaja (wa pili kushoto), mkurugenzi wa manunuzi wa Kundi la Kampuni za Uuzaji Bidhaa kwa Rejareja la Kawan Lama la Indonesia, akitembelea kwenye Maonyesho ya 135 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 16, 2024. (Xinhua/ Liu Dawei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma