Lugha Nyingine
Jukwaa la Kiumma la WTO 2024 lafuatilia “utandawazi wa uchumi wa dunia wa mara ya pili”
Tarehe 10, Septemba, 2024, Ngozi Okonjo-Iweala, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) (jukwaani) akihutubia Jukwaa la Kiumma la WTO 2024 huko Geneva, Uswisi. (Xinhua/Lian Yi)
Jukwaa la Kiumma la WTO 2024 limefunguliwa tarehe 10 huko Geneva, likiwa na kaulimbiu ya “Utandawazi wa Uchumi wa Dunia wa Mara ya Pili: Biashara Nzuri Zaidi, Dunia Nzuri Zaidi”.
Shughuli ya mwaka huu inalenga kujadili namna gani utandawazi wa uchumi wa dunia wa mara ya pili unaweza kuifanya biashara iwe jumuishi zaidi na kuhakikisha watu wengi zaidi wananufaika nao.
Mkurugenzi mkuu Ngozi Okonjo-Iweala alinukuu matokeo kwenye toleo la 2024 la “Ripoti ya Biashara Duniani” iliyotolewa hivi karibuni akisema kuwa, biashara za kimataifa zinasaidia kupunguza pengo la mapato kati ya makundi mbalimbali ya uchumi, na kuhimiza ujumuishi wa uchumi wa dunia.
Okonjo-Iweala alisema, kuanzia mwaka 1995 hadi 2023, baada ya kuondoa athari ya mfumuko wa bei, wastani wa mapato ya kila mtu duniani umeongezeka kwa asilimia 65 hivi; Huku wastani wa mapato ya kila mtu wa makundi ya uchumi yenye mapato ya kati na ya chini umeongezeka karibu maradufu.
Alisema, “Tangu Mapinduzi ya Viwanda yalipofanyika, nchi maskini zimepunguza kwa mara ya kwanza pengo la mapato kati yao na nchi tajiri.”
Lakini mkurugenzi mkuu huyo aliongeza kuwa, nchi nyingi maskini, hasa nchi za Afrika, Latin Amerika na Mashariki ya Kati bado zipo ukingoni mwa biashara za dunia.
Okonjo-Iweala alisisitiza kuwa, kujilinda kiuchumi si njia yenye ufanisi ya kutimiza ujumuishi. Badala yake kufanya biashara nyingi zaidi na biashara nzuri zaidi ndiyo njia ya kuwafanya watu na maeneo yaliyopo ukiongoni kuingia kwenye mkondo mkuu wa uchumi wa dunia.
Jukwaa hilo la siku nne litafanya mikutano 138, na limevutia washiriki karibu 4,400 kutoka serikali, kampuni, sekta ya wanataaluma na watu wa sekta mbalimbali za jamii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma