Lugha Nyingine
Benki Kuu ya Marekani yapunguza viwango vya riba kwa alama 50, ikiwa ni mara ya kwanza katika miaka minne
Benki Kuu ya Serikali ya Marekani imepunguza viwango vya riba kwa alama 50 siku ya Jumatano kufuatia kupungua kwa mfumuko wa bei na kudhoofika kwa soko la ajira, ikiashiria kupunguzwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minne.
Kamati ya Serikali ya Soko Wazi (FOMC) imesema katika taarifa yake kwamba, kamati hiyo imepata imani kubwa zaidi kutokana na mfumuko wa bei kuendelea kushuka kuelekea asilimia 2, na hatari za kufikia malengo yake ya ajira na mfumuko wa bei zikiwa karibu katika uwiano.
Hivyo kwa kuzingatia maendeleo hayo, kamati imeiamua kupunguza lengo lake la kiwango cha fedha za serikali kwa alama 50 kuwa asilimia 4.75 hadi asilimia 5.
Baada ya kudumisha viwango vya juu kwa zaidi ya mwaka mmoja, sera kali ya fedha ya serikali ilikabiliwa na shinikizo la kubadilika kutokana na kupunguza shinikizo la mfumuko wa bei, ikiashiria kudhoofika kwa soko la ajira, na kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma