Lugha Nyingine
China yarusha satalaiti mbili za BeiDou?za uongozaji wa?usafiri
Satalaiti za 59 na 60 za mfumo wa BeiDou zikirushwa majira ya saa 3:14 asubuhi (kwa saa za Beijing) kwa roketi ya kubeba ya Long March-3B na Yuanzheng-1 (Expedition-1) ya ngazi ya juu ikiwa imeunganishwa kwenye roketi hiyo ya kubeba kutoka kwenye Kituo cha Urushaji Satalaiti cha Xichang katika Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, Septemba 19, 2024. (Picha na Yang Xi/Xinhua)
XICHANG - China imerusha satalaiti mbili mpya za Mfumo wa Satalaiti za BeiDou-3 (BDS-3) za uongozaji wa usafiri siku ya Alhamisi kwenda anga ya juu kutoka Kituo cha Kurusha Satalaiti cha Xichang katika Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China ambapo satalaiti hizo mbili, ya 59 na 60 za mfumo wa satalaiti za BeiDou, zimerushwa majira ya saa 3:14 asubuhi (kwa saa za Beijing) kwa roketi ya kubeba ya Long March-3B na Yuanzheng-1 (Expedition-1) ya ngazi ya juu ikiwa imeunganishwa kwenye roketi hiyo ya kubeba.
Ni kundi la pili la satalaiti za obiti ya kati ya Dunia (MEO) kurushwa tangu mfumo wa BDS-3 ulipozinduliwa na kuanza kufanya kazi rasmi kutoa huduma za urambazaji za satalaiti duniani kote.
Baada ya kuingia kwenye obiti na kukamilisha majaribio ya obiti, zitaunganishwa kwenye mfumo wa BDS. Ikilinganishwa na kundi la awali la satalaiti za MEO, satalaiti hizi mpya zina saa za kiatomiki zilizoboreshwa na vituo vipya vya kuunganisha kati ya satalaiti.
Satalaiti hizo zitaboresha zaidi uhakika wa mfumo wa BDS-3 na ufanisi wa uwekaji, uongozaji wa usafiri na utoaji ishara ya saa sahihi za dunia (PNT), mawasiliano ya habari fupi za kote duniani na huduma zingine.
Satalaiti hizo pia zitatumika kwa majaribio ya teknolojia mpya kwa ajili ya mfumo wa kizazi kijacho cha satalaiti za BDS, Idara ya Uongozaji wa Usafiri wa Satalaiti ya China imesema.
Hili ni jukumu la 535 la kurusha satalaiti kwa roketi za kubeba za msururu wa Long March.
Satalaiti za 59 na 60 za mfumo wa BeiDou zikirushwa majira ya saa 3:14 asubuhi (kwa saa za Beijing) kwa roketi ya kubeba ya Long March-3B na Yuanzheng-1 (Expedition-1) ya ngazi ya juu ikiwa imeunganishwa kwenye roketi hiyo ya kubeba kutoka kwenye Kituo cha Urushaji Satalaiti cha Xichang katika Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, Septemba 19, 2024. (Picha na Yang Zhiyuan/Xinhua)
Satalaiti za 59 na 60 za BeiDou za uongozaji wa usafiri zikirushwa majira ya saa 3:14 asubuhi (kwa saa za Beijing) kwa roketi ya kubeba ya Long March-3B na Yuanzheng-1 (Expedition-1) ya ngazi ya juu ikiwa imeunganishwa kwenye roketi hiyo ya kubeba kutoka kwenye Kituo cha Urushaji Satalaiti cha Xichang katika Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, Septemba 19, 2024. (Picha na Yang Xi /Xinhua)
Satalaiti za 59 na 60 za BeiDou za uongozaji wa usafiri zikirushwa majira ya saa 3:14 asubuhi (kwa saa za Beijing) kwa roketi ya kubeba ya Long March-3B na Yuanzheng-1 (Expedition-1) ya ngazi ya juu ikiwa imeunganishwa kwenye roketi hiyo ya kubeba kutoka kwenye Kituo cha Urushaji Satalaiti cha Xichang katika Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, Septemba 19, 2024. (Picha na Yang Zhiyuan/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma