Lugha Nyingine
China yatoa wito wa juhudi za pamoja za kuhimiza usimamizi wa Dunia
Wang Yi, mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na waziri wa mambo ya nje wa China, akihutubia kwenye Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Mataifa wa Siku za Baadaye kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Septemba 23, 2024. (Xinhua/Xie E)
UMOJA WA MATAIFA - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa "kutunza vizuri maskani yetu ya pamoja" na kufanya juhudi za pamoja ili kuhimiza usimamizi wa Dunia, kwani "binadamu ana sayari moja tu ya Dunia inayoiita maskani, na tunatoka kwenye jumuiya sawa ya Dunia."
Tukikabiliana na mabadiliko makubwa ambayo hayakutokea katika miaka 100 iliyopita, ni muhimu sana kwamba viongozi wa Dunia wanakusanyika kwenye Mkutano wa Kilele wa Siku za Baadaye na, kwa pamoja, kupitisha “Mkataba wa Siku za Baadaye” ili kuchochea juhudi zao za pamoja kwa ajili ya amani na maendeleo ya Dunia, na kuweka dira ya mustakabali wa binadamu wa baadaye , amesema Wang, ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China na mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), katika hotuba yake kwenye mkutano huo.
Wang ameeleza kuwa kwa kutilia maanani lengo hilo, Rais Xi ameweka mbele maono ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, kutetea kujenga pamoja kwa sifa bora Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kutoa mapendekezo kuhusu Maendeleo ya Dunia, Usalama wa Dunia na Ustaarabu wa Dunia.
Wang amesema, maono na mapendekezo hayo, yametoa mipango mipya kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za pamoja za binadamu na kuweka dira mpya ya kujenga Dunia bora.
Waziri huyo amefafanua pendekezo lenye mambo manne lililotolewa na China. Kwanza, nchi za Dunia zinapaswa kujenga siku za baadaye zenye amani na utulivu, pili, nchi za Dunia zinapaswa kujenga siku za baadaye zenye maendeleo na ustawi, tatu, nchi za Dunia zinapaswa kujenga siku za baadaye zenye haki na usawa, na nne, nchi za Dunia zinahitaji kuendana na wakati na kujenga siku za baadaye zenye haki na halali zaidi.
Wang Yi, mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na waziri wa mambo ya nje wa China, akihudhuria Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Mataifa wa Siku za Baadaye kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Septemba 23, 2024. (Xinhua/Li Rui)
Wang Yi, mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na waziri wa mambo ya nje wa China, akihutubia kwenye Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Mataifa wa Siku za Baadaye kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Septemba 23, 2024. (Xinhua/Li Rui)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma