Lugha Nyingine
Shughuli mbalimbali za kitamaduni na utalii zitaongezwa wakati wa likizo ya Sikukuu ya Taifa
Watu wakitembelea Soko la Maua la Dounan wakati wa Sikukuu ya Jadi ya Mbalamwezi ya China na likizo ya Sikukuu ya Taifa ya China huko Kunming, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Oktoba 5, 2023. (Xinhua/Chen Xinbo)
BEIJING - China itaongeza shughuli za kitamaduni na bidhaa za utalii kabla na baada ya likizo ya wiki nzima ya Sikukuu ya Taifa ya China itakayoanza Oktoba Mosi, Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China (MCT) imetangaza Jumanne.
Hatua hiyo inalenga kukidhi mahitaji ya watu yanayoongezeka juu ya bidhaa za kitamaduni na utalii wakati wa likizo hiyo ijayo, wizara hiyo imesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Shughuli takriban 1,000 za kitamaduni zenye maudhui kuhusu mali za urithi wa utamaduni usioshikika zinatarajiwa kufanyika nchini kote China, amesema Hu Yan, afisa wa wizara hiyo.
Na sehemu za vivutio vya utalii pia zitaonesha mvuto wa mali za urithi wa utamaduni usioshikika. Kwa mfano, vitu kadhaa vinavyohusu mali za urithi wa utamaduni usioshikika vitapangwa kuonyeshwa katika Hekalu la Xiaoxitian kwenye sehemu ya kivutio cha utalii katika Mkoa wa Shanxi, kaskazini mwa China, Hu ameongeza.
Njia zaidi zinazohusika na utalii wa vijijini na kiikolojia pia zitakuwa wazi kwa ajili ya umma, wizara hiyo imesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma