超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

China na Russia zaadhimisha miaka 75 tangu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2024

Li Hongzhong, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akihudhuria hafla ya kusherehekea miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 25, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

Li Hongzhong, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akihudhuria hafla ya kusherehekea miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 25, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING - China imefanya hafla mjini Beijing siku ya Jumatano kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wake wa kidiplomasia na Russia ambapo makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, Li Hongzhong alihudhuria na kuhutubia hafla hiyo.

Li, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia, uhusiano wa pande mbili umestahimili majaribu ya nyakati na umekuwa thabiti.

Uhusiano kati ya China na Russia umekuwa ukisonga mbele kwa ngazi ya juu katika zama mpya, ambayo inachangiwa na uongozi na mwongozo wa viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, amesema.

China ina nia ya kufanya kazi na Russia, ikiongozwa na makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi hao wakuu wa nchi hizo mbili, ili kuimarisha kuaminiana kimkakati, kujenga kikamilifu mwelekeo mpya wa ushirikiano wa kunufaishana, kuongeza kuelewana na uhusiano kati ya watu wa nchi hizo mbili, na kulinda ustawi na utulivu wa kimataifa, Li ameongeza.

Kwa upande wake Balozi wa Russia nchini China Igor Morgulov amesema Russia ina nia ya kufanya kazi na China ili kutekeleza ipasavyo makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi hao wakuu wawili wa nchi na kuhimiza maendeleo endelevu ya uhusiano wa pande mbili.

Hafla hiyo imeandaliwa kwa pamoja na Shirikisho la Watu wa China kwa Urafiki na Nchi za Nje na Jumuiya ya Urafiki wa China na Russia. Wawakilishi takriban 300 kutoka nyanja mbalimbali za maisha nchini China na Russia wamehudhuria hafla hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha