Lugha Nyingine
Rais Xi atoa heshima kwa mashujaa waliofariki dunia katika Siku ya Wahanga
Xi Jinping akinyoosha utepe kwenye kikapu cha maua katika hafla ya kutoa vikapu vya maua kwa mashujaa waliofariki dunia iliyofanyika uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 30, 2024. (Xinhua/Wang Ye)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine wa chama na serikali Jumatatu walihudhuria hafla kwenye uwanja wa Tian'anmen katikati mwa Beijing kutoa vikapu vya maua kwa mashujaa waliofariki dunia ambapo hafla hiyo imefanyika kuadhimisha Siku ya Wahanga, ambayo huadhimishwa siku moja kabla ya Sikukuu ya Kitaifa ya China ambayo inaadhimisha leo Oktoba Mosi.
Mwaka huu, China inaadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China (PRC).
Majira ya saa 4 asubuhi, Rais Xi na viongozi wengine -- Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng -- walifika kwenye uwanja huo. Walijumuika pamoja na wawakilishi kutoka nyanja zote za maisha.
Miongoni mwa wahudhuriaji zaidi ya 2,400 waliokuwa wameshika maua ni askari wastaafu, jamaa za wahanga, wapokeaji wa nishani na hadhi za heshima za kitaifa, watu wa mifano ya kuigwa, wanafunzi na watoto.
Hafla ilipoanza, wahudhuriaji wote waliimba wimbo wa taifa la China, ikifuatiwa na muda wa kukaa kimya kuwaenzi mashujaa waliojitoa maisha yao kwa ajili ya ukombozi wa watu wa China na maendeleo ya Jamhuri ya Watu wa China.
Vikapu tisa vikubwa vya maua, vikiwa na utepe uliosomeka "Utukufu wa Milele kwa Mashujaa wa Umma," viliwekwa mbele ya Mnara wa Mashujaa wa Umma.
Rais Xi na viongozi wengine walikaribia chini ya mnara huo, ambapo alinyoosha riboni kwenye vikapu kabla ya kuwaongoza maafisa wengine kutembea karibu na mnara huo kutoa heshima zao.
Haflla hiyo iliongozwa na Yin Li, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkuu wa Chama katika Mji wa Beijing.
Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama na serikali wakiwemo Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng wakihudhuria hafla ya kutoa vikapu vya maua kwa mashujaa waliofariki dunia iliyofanyika uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 30, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Xi Jinping akitembea karibu na Mnara wa Mashujaa wa Umma kutoa heshima katika hafla ya kutoa vikapu vya maua kwa mashujaa waliofariki dunia iliyofanyika uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 30, 2024. (Xinhua/Wang Ye)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma