Lugha Nyingine
China yashughulikia vifurushi takriban bilioni 6.3 wakati wa likizo ya Siku ya Taifa
Muonyeshaji bidhaa akitayarisha gari la kiotomatiki la usambazaji vifurushi lisiloendeshwa na dereva lililooneshwa kwenye Maonyesho ya Teknolojia za Akili Mnemba Duniani Mwaka 2024 mjini Tianjin, Kaskazini mwa China, Juni 20, 2024. (Xinhua/Sun Fanyue)
BEIJING – Tasnia ya posta na usambazaji haraka wa vifurushi nchini China imeshughulikia vifurushi bilioni 6.3 wakati wa likizo ya siku saba ya Siku ya Taifa iliyomalizika Jumatatu wiki hii, ikionyesha kushamiri kwa shughuli za utalii na matumizi katika kipindi hicho.
Takwimu zilizotolewa na Shirika la Posta la Serikali ya China siku ya Jumanne zimeonesha kuwa, Vifurushi jumla ya bilioni 3.16 vilikusanywa wakati wa likizo hiyo, huku wastani wa makusanyo ya vifurushi ya kila siku ukiongezeka kwa asilimia 28.4 ikilinganishwa na ule wa kipindi kama hicho cha mwaka jana.
Idadi ya vifurushi vilivyowasilishwa ilifikia jumla ya bilioni 3.12, na kiasi cha kila siku cha vifurushi vilivyowasilishwa kiliongezeka kwa asilimia 26.7 kuliko Mwaka 2023.
Kampuni husika zimechukua hatua mbalimbali ili kukidhi mahitaji makubwa nchini kote, ikiwa ni pamoja na kuongeza muda wa huduma na kushirikiana na kampuni za utamaduni na utalii, shirika hilo limesema.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma