Lugha Nyingine
Africa CDC yatoa wito wa kutengeneza vifaa tiba kwa ajili ya maandalizi ya mlipuko wa maradhi
(CRI Online) Oktoba 10, 2024
Mkurugenzi wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) Jean Kaseya ameeleza wasiwasi wake juu ya Afrika kutegemea msaada wa nje kwenye vifaa tiba wakati wa kipindi cha mlipuko wa maradhi.
Akihutubia siku ya Jumatano Kongamano la Biashara la Eneo la Biashara Huria la Afrika lililofanyika mjini Kigali nchini Rwanda, Kaseya amesisitiza kuwa Afrika inahitaji kujitegemea katika kutengeneza chanjo, dawa na uchunguzi wa ugonjwa.
Kaseya ameongeza kuwa kila linapotokea janga, Afrika huingiwa na hofu, hali ambayo inalilazimisha bara hilo lianze kuomba chanjo, dawa na uchunguzi wa magonjwa kutoka nje.
Ametoa wito wa kuchukua hatua mara moja kutengeneza vifaa tiba ndani ya Afrika.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma