Lugha Nyingine
Uganda yaadhimisha miaka 62 tangu ipate uhuru
Wakati Uganda ikifanya maadhimisho ya miaka 62 tangu ujipatie uhuru kutoka kwa wakoloni wa Uingereza yaliyofanyika katika wilaya ya Busia mashariki mwa Uganda, Rais Yoweri Museveni ametoa wito wa uzalishaji mali, na kusisitiza ongezeko la thamani katika mazao ya kilimo.
Rais Museveni amesema kuwa tatizo la Afrika na nchi nyingine zilizokuwa makoloni ni kujikita katika kuzalisha malighafi pekee, jambo ambalo limekuwa na madhara kwa bara hilo, akibainisha kuwa Uganda imeongeza thamani ya bidhaa zake kwa makusudi ili kuingiza mapato zaidi yatokanayo na mauzo ya nje.
Ameongeza kuwa chini ya mipango mbalimbali ya maendeleo ya serikali, asilimia takriban 67 ya wakazi wa Uganda sasa wanashiriki katika uchumi wa fedha.
Rais Faustin-Archange Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya Kati aliyefanya ziara nchini Uganda pia alishiriki kwenye sherehe hizo, akimpongeza Rais Museveni kwa uongozi wake, kwa sababu ameifanya Uganda kuwa nchi nzuri yenye maridhiano ya kitaifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma