超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Semina kuhusu?uhusiano kati ya China na Afrika yafanyika nchini Tunisia ili kuchunguza matarajio ya ushirikiano wa siku za baadaye

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 12, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia Mohamed Ben Ayed akizungumza kwenye semina yenye mada ya "China-Afrika: Fursa na Matarajio ya Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja kwa Nyakati Zote katika Zama Mpya" mjini Tunis, Tunisia, Oktoba 9, 2024. (Picha na Adel Ezzine/Xinhua)

TUNIS - Semina kuhusu fursa na matarajio ya ushirikiano kati ya China na Afrika yenye mada "China na Afrika: Fursa na Matarajio ya Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja kwa Nyakati Zote katika Zama Mpya" imefanyika mjini Tunis, Tunisia siku ya Jumatano ikiwa imeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia na Ubalozi wa China nchini Tunisia.

Kwenye semina hiyo iliyohudhuriwa na viongozi, wataalamu na wasomi kutoka Tunisia, China, Algeria, Morocco na nchi nyingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia Mohamed Ben Ayed ameeeleza imani yake katika ushirikiano wa siku za baadaye kati ya Tunisia na China na dhamira ya nchi yake katika "kuimarisha ushirikiano wake" na China.

"China ni rafiki mwaminifu wa Tunisia na nchi nyingine za Afrika. Juu ya msingi wa kuheshimiana na kunufaishana, China na Tunisia zimeanzisha uhusiano wa muda mrefu wa ushirikiano katika nyanja nyingi zikiwemo miundombinu, huduma za afya, elimu, michezo na teknolojia ya hali ya juu. "amesema.

Akibainisha kuwa China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea inayowekeza barani Afrika, Balozi wa China nchini Tunisia Wan Li amesema kwenye semina hiyo kuwa hadi mwishoni mwa Mwaka 2023, thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika ilizidi dola za kimarekani bilioni 40.

China imeendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa mwaka wa 15 mfululizo, na thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili ilifikia dola za Marekani bilioni 282.1 Mwaka 2023, Wan amesema.

Semina hiyo ilikuwa ni fursa nzuri ya kurejea mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Afrika kwani China imependekeza hatua 10 za ushirikiano kwa ajili ya ujenzi wa mambo ya kisasa ambazo itashirikiana na Afrika kuzichukua katika miaka mitatu ijayo.

Balozi wa China nchini Tunisia, Wan Li akizungumza kwenye semina yenye mada ya "China-Afrika: Fursa na Matarajio ya Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja kwa Nyakati Zote katika Zama Mpya" mjini Tunis, Tunisia, Oktoba 9, 2024. (Picha na Adel Ezzine/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha