Lugha Nyingine
China yafuatilia maendeleo ya hali ya Peninsula ya Korea
Vyombo vya habari vya Jamhuri ya Korea vimeripoti kuwa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) imelipua sehemu ya barabara kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Jamhuri ya Korea.
Akizungumzia suala hilo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema, China ikiwa nchi jirani ya Peninsula ya Korea, inafuatilia maendeleo ya hali ya Peninsula hiyo na mwelekeo wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Pia amesema hali hiyo ya wasiwasi kwenye Peninsula hiyo haiendani na maslahi ya pamoja ya pande zote, na kwamba kazi kuu kwa sasa ni kuepuka kuongezeka zaidi kwa mvutano.
Pia amesisitiza kuwa China siku zote inaunga mkono kulinda amani na utulivu wa Peninsula ya Korea na kwamba msimamo wake wa kuhimiza ufumbuzi wa kisiasa wa suala la Peninsula hiyo haubadiliki, na inatumaini kuwa pande zote zitafanya juhudi za pamoja kufikia lengo hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma