超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Jeshi la Israel lathibitisha kumuua kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 18, 2024

Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa tarehe 1 Mei 2017 ikimuonyesha Yahya Sinwar (mbele) katika Mji wa Gaza. (Picha na Wissam Nassar/Xinhua)

Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa tarehe 1 Mei 2017 ikimuonyesha Yahya Sinwar (mbele) katika Mji wa Gaza. (Picha na Wissam Nassar/Xinhua)

JERUSALEM - Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) na Mamlaka ya Usalama ya Israel (ISA) kwa pamoja katika taarifa ya Alhamisi vimethibitisha kwamba kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar ameuawa na wanajeshi wa Israel katika Ukanda wa Gaza siku ya Jumatano, vikisema kuwa "Wanajeshi wa IDF kutoka Kamandi ya Kusini wamemwangamiza Yahya Sinwar... katika operesheni kusini mwa Ukanda wa Gaza,"

IDF imesema kwamba wanajeshi wake walikuwa wameua wanamgambo watatu katika operesheni hiyo, na baadaye, ikaja kujulikana kwamba mmoja wao ni Sinwar, ambaye "alihusika na mauaji na utekaji nyara wa Waisraeli wengi."

Taarifa hiyo imesema, Sinwar ameuawa baada ya kuwa akijificha mwaka mmoja uliopita nyuma ya raia wa Gaza, kote juu na chini ya ardhi, ndani ya mahandaki ya Hamas katika Ukanda wa Gaza.

"Operesheni nyingi zilizofanywa na IDF na ISA katika mwaka mmoja uliopita, na katika wiki za hivi karibuni kwenye eneo hilo ambalo ameuawa, zilizuia mijongeo ya kioperesheni ya Sinwar kwa kuwa alikuwa akifuatiliwa na vikosi na kupelekea kuangamizwa kwake huko," imeongeza taarifa hiyo.

Muda mfupi kabla ya taarifa ya IDF, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Israel Katz alithibitisha kifo cha Sinwar katika habari zilizotolewa naye kwa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi nyingine, akisema kuwa "haya ni mafanikio makubwa ya kijeshi na kimaadili kwa Israeli."

Waziri huyo wa mambo ya nje amesema, " kuangamizwa kwa Sinwar kunaleta uwezekano wa kuachiliwa mara moja kwa mateka wa Israel, na kuleta mabadiliko yatakayosababisha hali mpya halisi huko Gaza ya kutokuwa na udhibiti wa Hamas wala wa Iran."?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha