Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ampongeza Taneti Maamau kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Kiribati
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Taneti Maamau kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Kiribati. Kwenye salamu hizo za pongezi Rais Xi amesema China na Kiribati ni marafiki wazuri, washirika wazuri na ndugu wema.
Pia amesema tangu China na Kiribati zirudishe uhusiano wa kidiplomasia kati yao Septemba 2019, nchi hizo mbili zimeshuhudia kuongezeka kuaminiana kisiasa, ushirikiano wa kivitendo na mawasiliano ya karibu kati ya watu na kati ya ngazi za serikali za mitaa. Rais Xi akiongeza kuwa pande hizo mbili muda wote zimeelewana na kuungana mkono katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi na masuala makuu yanayofuatiliwa na kila upande.
Akibainisha kuwa anathamini maendeleo ya uhusiano kati ya China na Kiribati, Rais Xi amesema anapenda kushirikiana na Rais Maamau kuendeleza maendeleo thabiti na ya muda mrefu ya uhusiano kati ya pande hizo mbili ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma